Xscape
Xscape lilikuwa kundi la waimbaji wa kike wa R&B kutoka Atlanta, Georgia nchini Marekani. Kundi lilipata platinamu tatu mfululizo kwa albamu zao ikiwa ni pamoja na kushika nafasi ya 6 na kuingiza vibao 10 bab-kubwa katika chati za Billboard Hot 100 katika kipindi cha miaka ya 1990 - "Just Kickin' It", "Who Can I Run To", "The Arms of the One Who Loves You", na "My Little Secret". Kikosi halisi cha kundi kiliunganishwa na ndugu ambao ni LaTocha na Tamika Scott, Kandi Burruss, Tameka "Tiny" Cottle, na Tamera Coggins, lakini Coggins aliondoka kabla kundi halijatoa hata albamu yao ya kwanza.
Xscape | |
---|---|
Chimbuko | Atlanta, Georgia, U.S. |
Miaka ya kazi | 1991–2001; 2005–2009 |
Studio | So So Def/Columbia/SME Records (1992-1998) |
Ameshirikiana na | Bow Wow, Jermaine Dupri |
LaTocha Scott Tamika Scott Tameka "Tiny" Cottle Kandi Burruss Kiesha Miles Tamera Coggins-Wynn |
Historia
haririLaTocha na baba wa Tamika Scott, Rev. Randolf Scott, walikuwa sehemu ya kundi la R&B Scott Three mwanzoni mwa miaka ya 1970. Ndugu hawa walifundishwa kuimba na baba yao wkaiwa katika umri mdogo kabisa. Wanaimba kanisani na baadaye wanaenda kwenye mashindano ya watoto wenye vipaji huku wakikua. Mwanzoni mwa miaka ya 1990, wakakutana na wanachama wengine watatu wa Xscape, Kandi Burruss, Tamera Coggins-Wynn, na Tameka "Tiny" Cottle katika tumbuizo la kisanaa la shulel, Tri-Cities, huko mjini East Point, Georgia, nje kidogo ya mjini wa Atlanta. Baba wa Cottle, Charles Pope, na mjomba'ke, Joseph Pope (1933–1996), walikuwa wanachama wa kundi la R&B, The Tams.
Diskografia
haririStudio albamu
hariri- 1993: Hummin' Comin' at 'Cha
- 1995: Off the Hook
- 1998: Traces of My Lipstick
Marejeo
haririViungo vya Nje
haririBook: Xscape | |
Wikipedia books are collections of articles that can be downloaded or ordered in print. |