Youssou N'Dour
Youssou N'Dour (amezaliwa 1 Oktoba, 1959) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki maarufu kutoka Senegal. Anajulikana kimataifa kwa sauti yake ya kipekee na mchango wake katika muziki wa Afrika. Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni pamoja na 7 Seconds (1994) - ft. Neneh Cherry, Birima (2000), Nelson Mandela (1986), Ob-La-Di, Ob-La-Da (1995) (cover ya Beatles), Set (1990), Shaking the Tree (1990) - ft. Peter Gabriel, New Africa (1989), Medina (1997), My Hope is in You (1994) na Africa Dream Again (1996).
Youssou N'Dour | |
---|---|
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | Youssou N'Dour |
Amezaliwa | 1 Oktoba 1959 Dakar, Senegal |
Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwanamuziki |
Ala | Sauti, gitaa |
Miaka ya kazi | 1979 - sasa |
Ameshirikiana na | Super Étoile de Dakar |
Wavuti | Official website |
Muziki na maisha
haririYoussou N'Dour alianza kufanya muziki katika miaka ya 1970 akiwa kijana. Alianzisha bendi yake ya kwanza, Super Étoile de Dakar, ambayo ilichochea ukuaji wa aina ya muziki wa "Mbalax." Muziki ambao ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa Senegal na muziki wa kisasa.
Baadaye, N'Dour alipata umaarufu ulimwenguni kwa kipawa chake cha sauti yake ya kipekee. Pia kuweza kuchanganya mitindo mbalimbali ya muziki. Aliendelea kutoa albamu nyingi zilizofanikiwa, ambazo zilimfanya awe mmoja wa wanamuziki mashuhuri kutoka Afrika.
Katika safari yake ya kumuziki, amefanikiwa kujishindia tuzo mbalilimbali. Ikiwa ni pamoja na Grammy kwa albamu zake za "Egypt" na "Rokku Mi Rokka," ambazo zilikuwa na athari kubwa kwa tasnia ya muziki wa dunia. Pia amekuwa balozi wa utamaduni wa Senegal ulimwenguni kote.
Siasa
haririMbali na muziki, Youssou N'Dour amewahi kujihusisha sana na siasa na shughuli za kijamii nchini Senegal. Alijitupa katika kinyang'nyiro cha kuwania urais wa Senegal mwaka 2012, akigombea dhidi ya rais wa wakati huo, Abdoulaye Wade.
Diskografia
haririBaadhi ya albamu maarufu za Youssou N'Dour ni pamoja na:
- Immigrés (1984)
- The Lion (1989)
- Eyes Open (1992)
- Egypt (2004)
- Rokku Mi Rokka (2007)
Marejeo
hariri- *Biography of Youssou N'Dour* - BBC News
- *Youssou N'Dour: The Voice of Senegal* - CNN
- *Official Website of Youssou N'Dour Ilihifadhiwa 21 Februari 2024 kwenye Wayback Machine.*
Viungo vya Nje
hariri- Official Website of Youssou N'Dour Ilihifadhiwa 21 Februari 2024 kwenye Wayback Machine.
- Youssou N'Dour on YouTube
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Youssou N'Dour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari. |