Zaina Foundation ni asasi isiyo ya kiserikali na ya kifaida iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2017 ikiwalenga sana wanawake na watoto wa kike katika kuwawezesha juu ya matumizi sahihi ya mitandao na mifumo ya kidijitali [1]

Taasisi hii imekuwa ikiandaa mafunzo na semina mbalimbali kwa wanawake na watoto wa kike juu ya namna ya kutumia ulinzi katika mitandao ili kujikinga na unyanyasaji wa kijinsia [2] na ulinzi wa kimtandao.

Malengo hariri

Kuwezesha wasichana na wanawake katika teknolojia kupitia usalama wa dijiti na semina za kujenga uwezo wa faragha na mafunzo.

Maono hariri

Kuendeleza na kusaidia wanawake ambao ni waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, wanafunzi wa teknolojia, wanasheria, na wanafunzi sawa, kuboresha kabisa njia pamoja na kulinda taarifa za mitandaoni.

Taasisi hiyo ilianzishwa na Zaituni Njovu ambaye ni mtaalamu wa teknolojia za habari na mawasiliano [3].

Tanbihi hariri

  1. "About Us – Zaina Foundation" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2020-02-09. 
  2. helen. "Zaina Foundation increasing cyber security knowledge for Tanzanian women". Safe Sisters (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-08-12. Iliwekwa mnamo 2020-02-09. 
  3. "CIPESA-FIFAfrica2019-Zaituni". Forum on Internet Freedom in Africa (FIFAfrica) (kwa en-US). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-18. Iliwekwa mnamo 2020-02-09.