Zipporah Kittony
Zipporah Jepchirchir Kittony (alizaliwa 1943), anayejulikana zaidi kama Zipporah Kittony, ni mwanasiasa wa zamani wa Kenya na mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto. Alihudumu kama Mbunge aliyeteuliwa kati ya 1988 na 2007 na kama Seneta aliyeteuliwa na KANU kati ya 2013 na 2018. Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake (MYWO) kuanzia 1996 hadi 2006.[1]
Marejeo
hariri- ↑ Kibet, Lonah. "Zipporah Kittony:Her dedicated service to women and youth". Evewoman Magazine.
Makala hii kuhusu mwanasiasa huyo wa Kenya bado ni mbegu. Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |