Ziwa Nakuru ni mojawapo ya maziwa ya magadi katika Bonde la Ufa. Linapatikana kusini mwa mji wa Nakuru, katika eneo la kati nchini Kenya na linazungukwa na Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru. Hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1961. Ilianza ndogo, ikizingira ziwa hilo maarufu na maeneo ya milima yaliyo karibu. Na sasa imeongezwa kujumuisha sehemu kubwa ya maeneo ya mbuga.

Ziwa Nakuru
Nchi zinazopakana Kenya
Eneo la maji 5 to 45 km²

Wingi wa mwani katika ziwa hili huvutia kwa kiasi kikubwa ndege aina ya flamingo ambayo hupatikana sana katika ufuo wa ziwa hili.

Ndege wengine pia hustawi katika eneo hili, na hata wanyamapori wakubwa.

Mito inayoingia ziwani ni: mto Enchorro, mto Enderit, mto Isirkon, mto Lamuriak na mmojawapo kati ya mito inayoitwa mto Makalia. Kiwango cha maji katika ziwa hili kilishuka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya 1990 lakini hivi karibuni kimeweza kurejea kiwango cha kale.

Maana ya Nakuru ni "vumbi" au "Mahali pa vumbi" katika lugha ya Kimaasai.

Ziwa Nakuru imelindwa chini ya Mkataba wa Ramsar ya maeneo ya maji.

Mbuga ya Wanyama ya Kitaifa ya Ziwa Nakuru

hariri
 
Flamingo wakila katika Ziwa Nakuru

Mbuga ya kitaifa ya Wanyama ya Ziwa Nakuru (188 km ²), ilianzishwa mwaka 1961 kuzunguka Ziwa Nakuru, karibu na mji wa Nakuru. Inajulikana sana kwa maelfu, wakati mwingine mamilioni ya ndege aina ya flamingo yanayokusanyaka ufuoni mwa ziwa Nakuru. Ya usawa wa ziwa vifupi recog Idadi ya flamingo katika ziwa hutegemea maji na hali ya chakula na pahali bora kuwatazama ni juu ya kiinuko kinachoitwa Baboon Cliff. Eneo lingine lenye kivutio ni eneo la 188 km ambalo limezingirwa kwa ukuta wa seng'enge kuhifadhi wanyama walio na hatari ya kuangamia kama twiga , Kifaru mweusi na Kifaru mweupe

Hifadhi hii ya wanyama hivi karibuni imepanuliwa kupatia hifadhi Kiporu mweusi ili kuwazuia wawindaji haramu kuwavamia. Im Hifadhi maandamano kwa

Hifadhi hii ya wanyama sasa (2009) ina zaidi ya vifaru weusi 25, moja ya viwango vya ukubwa nchini, pamoja na takriban vifaru weupe 70. Pia kuna idadi fulani ya twiga aina ya Rothschild, ambazo ziliamishwa kwa usalama kutoka magharibi mwa Kenya mwanzo wa mwaka 1977. Waterbuck ni ya k Kati ya wanyama wanaokula wenzao ni simba na chui, lakini ni chui ambayo imekuwa ikionekana sana hivi karibuni. Hifadhi hii pia ina nyoka wakubwa ambao wanaishi ndani ya msitu na uonekana ya kivuka barabara ama kurukaruka mitini.

Makazi na wanyamapori

hariri

Ziwa Nakuru, ziwa ndogo yenye maji ya chumvi kusini mwa mji wa Nakuru inapatikana takriba kilomita 160 kutoka Nairobi. Hivyo basi inaweza kutumbelewa katika ziara ya siku moja kutoka mji mkuu.Au zaidi, kama sehemu ya mzunguko inayohusisha Masai Mara au Ziwa Baringo na Samburu mashariki. Ziwa hili ni maarufu sana duniani kama eneo kubwa ya kusanyiko ya ndege aina ya flamingo ambayo idadi yao ni zaidi ya milioni moja- ama hata milioni mbili!Wao hula mwani, ambayo hupatitakana kwa wingi katika ziwa hili.

Wanasayansi wanadhani kuwa flamingo hawa hula takribani kilo 250,000 za mwani kwa kila hekari kila mwaka. Kuna spishi aina mbili ya flamingo; flamingo wale wadogo wanaweza kutofautishwa kwani wana rangi nyekundu nene na ya pinki. Wale flamingo wakubwa wana busu yenye ncha nyeusi. Flamingo wale wadogo ndio ambao huonyeshwa kwenya filamu mara nyingi kwani idadi yao ni kubwa. Idadi ya flamingo imekuwa ikipungua hivi karibuni. Labda ni kwa sababu ya kuongeza kwa watalii,uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na viwanda ambavyo vina tupa takataka kwenye maji haya au maji yamebadilika yakawa hayafai kwa maisha. Kawaida, ziwa hupungukiwa na maji wakati wa kiangazi na hufurika wakati wa masika. Hivi karibuni,kumekuwa na tofauti baina ya kiwango cha maji wakati wa kiangazi na wakati wa mvua. Hii imekisiwa kutokana na kuangezeka kwa kubadilisha maeneo muhimu ya uhifadhi wa maji kuwa maneo ya ukulima wa dhati na maendelo mengineyo. Uchafuzi wa mazingara pia unaharibu chakula cha flamingo na kuwasababisha kuhamia maziwa ya karibu yakiwemo: Elmenteita, Simbi Nyaima na Bogoria. Badiliko ya anga ya eneo hili pia imekisiwa kuchangia mabadiliko kwenye mazingira ya eneo hili. Ripoti za vyombo vya habari hivi karibuni zimeashiria wasiwasi uliopo baina ya washika dau kufuatia uhamaji mkuu wa flamingo na pia vifo baina yao huenda ikasababisha hasara kubwa kwenye sekta ya utalii.

Flamingo hula mwani ambayo hotokana na mchanganyiko wa kiniesi chao pamoja na maji ya chumvi yaliyo vuguvugu pamoja na chakula cha samaki aina ya plankton. Lakini flamingo sio ndege wa kipekee wa kuvutia kwenye ziwa hili, kunao ndege wala samaki wa aina ya pelican na cormorants.Licha ya maji haya kuwa ya chumvi na vuguvugu,samaki aina ya Tilapia grahami imeonekana kunawiri baada ya kuwekwa mwanzo wa miaka ya 1960. Ziwa hili lina ndege wengi sana. Kuna zaidi ya spishi 400 kwenye ziwa hili na mbuga iizungukayo. Maelfu ya ndege wa aina nyingine pia huonekana. Kunao pia punda milia.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: