Alama ya swali
(Elekezwa kutoka ?)
Alama ya swali (ing. question mark) ni kati ya alama za vituo inayotumiwa kwenye mwisho wa sentensi wakati wa kuuliza swali. Umbo lake ni ?.
Asili ya alama
haririAlama hii imetokana na mwandiko wa Kilatini na inajulikana tangu karne ya 9 BK ilipoanza kupatikana kwenye maandiko yaliyotoka kwenye ofisi ya mfalme Karolo Mkuu.
Hakuna uhakika juu ya asili kamili lakini wataalamu wengi wanahisi ya kwamba waandishi walimaliza kila sentensi ya swali kwa neno "quaestio" (yaani "swali" kwa Kilatini). Neno hili lilifupishwa kwa kuandkia herufi za kwanza na za mwisho pekee hivyo: qo. Kifupi hiki kiliandikwa kwa kuweka herufi moja juu ya nyingine na herufi ya "q" haikufungwa tena.
Marejeo ya Nje
hariri- Lupton, Ellen and Miller, J. Abbott, "Period styles: a punctuated history", in The Norton Reader 11th edition, ed. Linda H. Peterson, Norton, 2003 Online excerpt (at least) Archived 14 Juni 2007 at the Wayback Machine.
- Parkes, M.B., Pause and Effect: an Introduction to the History of Punctuation in the West, University of California Press, 1993
- Truss, Lynne, Eats, Shoots & Leaves Gotham Books, NY, p. 139