18 (albamu)
18 ni albamu ya 2002 iliyofanya na msanii wa muziki wa mwenendo wa elektroniki Moby. Albamu hii inaashiria Moby akifuata mkondo wake wa awali katika albamu ya Play, ikishirikisha rekodi za nyanja za zamani za negro spirituals na kuziunganisha pamoja na midundo taratibu ya ‘’Dance’’. Hata hivyo, “18” ina tone ya huzuni zaidi ya Play . Albamu hii pia inaonyesha Moby akiingia katika mwenendo wa alternative rock ("We Are All Made of Stars", "Great Escape", "Extreme Ways", "Harbour"). Wimbo wenye mafanikio zaidi katika albamu hii ni single ya "We Are All Made of Stars", ambayo ilifika nafasi ya 11 katika chati za UK. Albamu hii inashirikisha wasanii spesheli kama Azure Ray, MC Lyte, Angie Stone, na Sinéad O'Connor. Mkusanyiko wa sehamu ya A na B na Video zilitolewa mwaka mmoja baada ya kutolewa kwa albamu hiyo katika 18 B Sides + DVD.
18 | ||
---|---|---|
Albamu ya Moby | ||
Imetolewa | 14 Mei 2002 | |
Urefu | 71:15 | |
Lebo | Mute - STUMM 202 V2 Records/ BMG |
Albamu hii ilianzia #1 katika chati za UK (Huk ikishinda ile ya Queen ya The Platinum Collection kutoka nafasi ya kwanza) na katika mataifa mengi ya Uropa. Pia ilifikia kilele katika nafasi ya 4 katika Billboard 200.
Mauzo yake yaliipa kiwango cha dhahabu na platinum katika zaidi ya mataifa 30 na iliuza zaidi ya nakala milioni 4 katika dunia nzima, ambalo lilikuwa jaribio bora sana kwa mwenendo wa elektroniki ambao haujulikani na wengi, ingawa idadi ya mauzo yake haikufikia hata nusu ya mauzo ya mtangulizi wake, blockbuster Play.
Mpangilio wa Vibao
hariri- "We Are All Made of Stars" – 4:32
- "In This World" (akimshirikisha Jennifer Price) – 4:02
- "In My Heart" – 4:36
- "Great Escape" (akimshirikisha Azure Ray) – 2:09
- "Signs of Love" – 4:25
- "One of These Mornings" (akimshirikisha Patti LaBelle) – 3:12
- "Another Woman" – 3:56
- "Fireworks" – 2:13
- "Extreme Ways" – 3:57
- "Jam for the Ladies" (akimshirikisha MC Lyte & Angie Stone) – 3:22
- "Sunday (The Day Before My Birthday)" – 5:09
- "18" – 4:28
- "Sleep Alone" – 4:45
- "At Least We Tried" (akishirikisha Freedom Bremner) – 4:08
- "Harbour" (akishirikisha Sinéad O'Connor) – 6:27
- "Look Back In" – 2:20
- "The Rafters" – 3:22
- "I'm Not Worried at All" – 4:11
Ngoma za Single
haririKuhusu Single |
---|
"We Are All Made of Stars"
|
"Extreme Ways"
|
"In This World"
|
"In My Heart" |
"Sunday (The Day Before My Birthday)"
|
"Jam for the Ladies"
|
Virejeleo
haririViungo vya Nje
hariri- 18 at MusicBrainz
Matumizi ya wimbo katika utamaduni maarufu
hariri- Wimbo "One Of These Mornings" ulitumiwa mwanzoni na mwishoni mwa Torchwood katika sehemu ya "To the Last Man," na pia katika sehemu chache za Without a Trace na pia katika filamu ya Miami Vice (2006).
- Wimbo "Extreme Ways" ulikuwa katika mwisho wa kila sehemu ya tamthilia ya Bourne movie.
Alitanguliwa na The Last Broadcast ya Doves |
UK number one album 25 Mei 2002 – 31 Mei 2002 |
Akafuatiwa na Destination ya Ronan Keating |
Alitanguliwa na Laundry Service ya Shakira |
Australian ARIA Albums Chart Albamu nambari moja 20 Mei – 26 Mei 2002 |
Akafuatiwa na The Eminem Show ya Eminem |