Ababu Namwamba
Pius Tawfiq Namwamba Ababu ni mwanasiasa wa Kenya. Mwanachama wa Orange Democratic Movement Namwamba alichaguliwa kuwakilisha Budalangi Constituency katika Bunge la Kenya katika uchaguzi wa ubunge wa Kenya, 2007.[1]
Ababu Namwamba ni Mwanasheria wa umma anayezingatia haki za binadamu za kimataifa na sheria ya kikatiba, na mwandishi wa gazeti mojawapo zinayoongoza nchini Kenya. Alizaliwa Uganda na wazazi waKenya na kukulia nchini Kenya.
Elimu
haririAbabu Namwamba alikuwa mwanafunzi wa Humphrey Fellowship (Fulbright) na ana digirii ya juu ya sheria katika Masomo ya sheria ya kimataifa kutoka Chuo kikuu cha Marekani cha sheria cha Washington, digirii ya juu ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na shahada ya sheria kutoka Shule ya Sheria ya Kenya.
Kazi ya Sheria
haririYeye ndiye mwanasheria mkuu katika Chambers of Justice, ambalo ni shirika la maslahi ya umma lililoanzishwa mwaka 2002. Yeye pia ana kampuni yake ya kisheria, Ababu Namwamba & Co mjini Nairobi, Kenya. Mheshimiwa Namwamba amechangia pakubwa katika mapambano ya kidemokrasia nchini Kenya, kutoka siku zake kama kiongozi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Tangu mwaka 2003, amekuwa akipigania demokrasia na utawala bora nchini Kenya katika mchakato wa utafiti ulioitwa "After the Promise", ambao unachambua utendaji wa serikali na watendaji wengine wa kisiasa.
Marejeo
hariri- ↑ wanachama wa Bunge 10. Ilihifadhiwa 16 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. Bunge la Kenya. Ilipatikana 1 Juni 2007.