Acarbose ni dawa inayotumika kutibu kisukari cha aina ya 2, pamoja na lishe na mazoezi.[1] Inaweza kutumika kwa wale ambao hawawezi kutumia metformin au kwa kuongeza dawa nyingine za ugonjwa wa kisukari.[1] Faida yake ni ndogo.[2] Inachukuliwa kwa mdomo kwa kila mlo.[1] Athari yake ya juu zaidi inaweza kuchukua wiki mbili.[1]

Acarbose
Haworth projection of acarbose
Ball-and-stick model of the acarbose molecule
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
O-4,6-Dideoxy-4-Kigezo:Bracket-α-D-glucopyranosyl-(1→4)-O-α-D-glucopyranosyl-(1→4)-D-glucopyranose
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Glucobay, Precose, Prandase, mengineyo
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a696015
Taarifa za leseni US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito B3(AU) B(US)
Hali ya kisheria POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kwa mdomo (vidonge)
Data ya utendakazi
Uingiaji katika mzunguko wa mwili Chini sana
Kimetaboliki Njia ya utumbo
Nusu uhai Masaa mawili
Utoaji wa uchafu Figo (chini ya 2%)
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe (2R,3R,4R,5S,6R)-5-{[(2R,3R,4R,5S,6R)-5- {[(2R,3R,4S,5S,6R)-3,4-dihydroxy-6-methyl- 5-{[(1S,4R,5S,6S)-4,5,6-trihydroxy-3- (hydroxymethyl)cyclohex-2-en-1-yl]amino} tetrahydro-2H-pyran-2-yl]oxy}-3,4-dihydroxy- 6-(hydroxymethyl)tetrahydro-2H-pyran-2-yl]oxy}- 6-(hydroxymethyl)tetrahydro-2H-pyran-2,3,4-triol
Data ya kikemikali
Fomyula C25H43NO18 
 YesY(Hiki ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuhara na kuongezeka kwa gesi ya matumbo.[1] Inapotumiwa peke yake, haileti sukari ya chini ya damu.[1] Madhara yake mengine ni pamoja na kuongezeka kwa vimeng'enya kwenye ini. [1] Haipendekezi kutumia kwa wale walio katika hatari ya kuziba matumbo.[2] Inafanya kazi kwa kupunguza kasi ya mmeng'enyo wa wanga (carbohydrates).[1]

Acarbose iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1995[1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Marekani, mwezi mmoja wa matumizi yake uligharimu takriban dola 16 kufikia mwaka wa 2021.[3] Nchini Uingereza, kiasi hiki kinagharimu NHS takriban pauni 15.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "Acarbose Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 18 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 729. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)
  3. 3.0 3.1 "Acarbose Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 18 Julai 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)