Lishe (kutoka kitenzi "kula" kikinyambuliwa kama "kulisha"; kwa Kiingereza: Nutrition) ni fani la sayansi ambalo hufafanua uwiano wa virutubishi na madini katika vyakula. Uwiano huu huangaliwa kati ya uzazi, kukua kwa kimo, afya na magonjwa.

Matunda mengi yanaboresha lishe.
Shoulder high portrait of white haired man with a mustache and beard wearing a suit and bow tie
Carl von Voit anahesabiwa kama baba wa lishe ya kisasa.

Lishe huhusisha kuliwa kwa chakula, madini na virutubishi kuchukuliwa mwilini, madini na virutubishi kutumiwa na seli za mwili, hali kadhalika kuondolewa kwa uchafu katika mwili.

Lishe ni chakula ambacho mnyama yeyote hula huambatana na jinsi kinavyopatikana. Katika binadamu lishe huhushisha maandalizi ya chakula, jinsi ya kukihifadhi na jinsi ya kuzuia chakula kupata hali mbovu ambayo yanaweza kuleta maradhi kwa binadamu.

Magonjwa yanayotokana na lishe hafifuEdit

Katika binadamu chakula chenye upungufu wa virutubishi na madini chaweza kusababisha maradhi kama vile upungufu wa damu mwilini, upofu, kutoka damu kwa fizi, kuzaliwa kwa mtoto kabla ya wakati kuwadia na mtoto kuzaliwa kama amekufa.

Chakula chenye wingi mkubwa mno wa virutubishi na madini chaweza kusababisha maradhi kama vile unene wa kupindukia, ugonjwa wa moyo, shinikizo la juu la damu pamoja na ugonjwa wa kisukari.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

 • Carpenter, Kenneth J. (1994). Protein and Energy: A Study of Changing Ideas in Nutrition. Cambridge University Press. ISBN 978-0521452090. 
 • Curley, S., and Mark (1990). The Natural Guide to Good Health, Lafayette, Louisiana, Supreme Publishing
 • Galdston, I. (1960). Human Nutrition Historic and Scientific. New York: International Universities Press. 
 • Gratzer, Walter [2005] (2006). Terrors of the Table: The Curious History of Nutrition. Oxford University Press. ISBN 978-0199205639. 
 • Mahan, L.K. and Escott-Stump, S. eds. (2000). Krause's Food, Nutrition, and Diet Therapy, 10th, Philadelphia: W.B. Saunders Harcourt Brace. ISBN 978-0-7216-7904-4. 
 • Thiollet, J.-P. (2001). Vitamines & minéraux. Paris: Anagramme. 
 • Walter C. Willett; Meir J. Stampfer (January 2003). "Rebuilding the Food Pyramid". Scientific American 288 (1): 64–71. doi:10.1038/scientificamerican0103-64
   . PMID 12506426
   .

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lishe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.