Acer predator 21x

kompyuta inayorandana na acer predator 21x
aer predator

Acer Predator 21x ni kompyuta mpakato kubwa kuliko nyingine kwa wakati wa sasa.

Kompyuta hii ina feni tano zinazosaidia kupunguza joto wakati kifaa hiki kinapokuwa kimewashwa. Kompyuta hii ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja na kwa ufanisi pia inaweza kuendesha michezo mbalimbali ya kielektroniki bila kukwamakwama.

Kompyuta hii inatengenezwa nchini Thailand na mpaka sasa inapatikana sehemu nyingi ulimwenguni na kwa kuwa ina uwezo mkubwa katika kazi inauzwa bei ghali.

Kompyuta hii haikai na chaji muda mrefu kwani inatumia umeme mwingi, hivyo muda mwingi inatakiwa kuwa imechomekwa kwenye umeme, tofauti na kompyuta mpakato nyingine ambazo hukaaa na chaji muda mrefu.