Acta Sanctorum
Acta Sanctorum (kwa Kilatini maana yake ni "Matendo ya Watakatifu") ni kamusi elezo ya Watakatifu wa Kanisa Katoliki inayofuata tarehe ya sikukuu yao.
Ni vitabu vikubwa 68 vilivyoandikwa huko Ubelgiji kwa kuzingatia ukweli wa historia kati ya karne ya 16 na karne ya 20 na kuchapwa kuanzia mwaka 1643 hadi 1940.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Acta Sanctorum kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |