Tarehe (kutoka Kiarabu تاریخ tarih kwa maana ya "historia") ni namna ya kutaja historia, lakini kwa kawaida zaidi nafasi ya siku fulani ndani ya mfumo wa kalenda.

Kwa kawaida tarehe inarejelea kalenda ya Gregori. Lakini ilhali kuna kalenda mbalimbali inawezekana kutaja na tarehe tofauti kwa siku ileile kutegemeana na kalenda inayorejelewa.

Tarehe za siku - mwezi - mwaka hariri

Tarehe hutaja mara nyingi sifa tatu za siku fulani:

Mfano: Sikukuu ya kwanza ya Jamhuri nchini Kenya ilitokea tarehe 12 Desemba 1963.

Tarehe za siku ya wiki hariri

Hasa katika biashara kuna pia namna tofauti ya kutaja tarehe kwa namba ya siku katika wiki halafu namba ya wiki katika mwaka. Mfumo huu unategemea mapatano katika nchi kuhusu namna ya kuhesabu siku, ipi ni siku ya kwanza na wiki gani ni wiki ya kwanza.

Tarehe kutegemeana na sikukuu hariri

Katika dini kuna pia namna ya kutaja tarehe kufuatana na sikukuu na hii kawaida katika mwaka wa liturujia katika makanisa mengi. Hapa kuna hesabu za Jumapili katika vipindi kama Kwaresima au Adventi, au baada ya sikukuu muhimu.

Mifano:

  • Jumapili ya tatu baada ya Pasaka
  • Jumapili ya kwanza ya Adventi

Tarehe mbalimbali kandoni hariri

Katika nchi ambako zinatumika kalenda za kitaifa zilizo tofauti na Kalenda ya Gregori ni kawaida kuonyesha kalenda kandoni. Kwa mfano nchini Iran mwaka unaanza kwa tarehe 1 mwezi wa Farwardin ambayo kwa kawaida ni sawa na 21 Aprili. Hivyo tarehe ya Kiirani 23 Farwardin 1396 ni sawa na tarehe 11 Aprili 2017. Ilhali nchini Iran hesabu ya kalenda ya Kiislamu ni muhimu kwa sikukuu za kidini kalenda za huko huonyesha pia tarehe ya tatu yaani 14 Rajabu 1438[1].

Kwa jumla nchi kadhaa za Kiislamu hutumia kalenda ya Kiislamu kando ya kalenda ya kimataifa ya Gregori.

Hii inafanana na nchi ya Israeli ambako tarehe za kalenda ya Kiyahudi zinaonyeshwa mara nyingi pamoja na tarehe za kalenda ya Gregori.

Tanbihi hariri

  1. Linganisha hapa tovuti ya kalenda ya Iran

Viungo vya Nje hariri