Adowa

(Elekezwa kutoka Adwa)

Adowa (pia: Adwa, Adua) ni mji wa Ethiopia karibu na mpaka wa Eritrea. Adowa ni sehemu ya mkoa wa Tigray katika nyanda za juu za Ethiopia kwa kimo cha mita 1,900. Mwaka 2016 ulikuwa na wakazi 63,759.

Mazingira karibu na Adowa

Historia

hariri

Umri wa mji wa Adowa haujulikani. Mji ulipata umaarufu fulani tangu kuanzishwa kwa mji mkuu Gondar kama kituo muhimu njiani kati ya pwani na Gondar maana wasafiri wote kutoka pwani walipita hapa. Mnamo mwaka 1700 ilikuwa makao ya gavana wa jimbo la Tigray ikawa mi muhimu aidi katika kaskazini ya Ethiopia. Soko lake lilijulikana na wakati wa karne ya 19 kulikuwa na jumuiya ya wafanyabiashara Wagiriki.

Adowa ilijulikana hasa kimataifa kutokana na mapigano ya Adowa ambako mwaka 1896 jeshi la Negus Menelik II ilishinda uvamizi wa Waitalia chini ya jenerali Oreste Baratieri. Ushindi huu ulizuia jaribio la Italia kuifanya Ethiopia kuwa koloni yake ikahakikisha uhuru wa Ethiopia.

Mwaka 1935 Adowa ilivamiwa na jeshi la Italia wakati wa vita ya pili kati ya Italia na Ethiopia. Waitalia walijenga kumbukumbu ya wafu wao wa 1896 lakini mwaka 1841 Waitalia walifukuzwa katika Eritrea na wanajeshi Wahindi wa jeshi la Uingereza waati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Takwimu

hariri

Kutokana na takwimu za idara kuu ya takwimu ya Ethiopia za mwaka 2016, Adowa ilikuwa na wakazi 63,759. Wakati wa zoezi la sensa ya mwaka 1994, ilirekodiwa jumla ya idadi ya watu kuwa ni 24,519.

Michezo

hariri

Timu ya mpira wa miguu ya Imeda iliweza kuwa timu ya taifa ya Ethiopia baada ya kushinda katika mashindano ya nyumbani

Filamu

hariri

Adwa (1999). ikiongozwa na Haile Gerima

Watu Muhimu

hariri

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Adowa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.