Akili bandia ya jumla

Akili bandia ya jumla (kutoka kwenye kiingereza Artificial General Intelligence au AGI kwa kifupi) ni tafiti ya kinadharia ya akili bandia inayojaribu kuunda programu ya kompyuta yenye utashi wa kibinadamu na zaidi, yenye uwezo wa kujifundisha yenyewe. Lengo la tafiti hii ni kuunda programu ya kompyuta yenye uwezo wa kufanya kazi ambazo haikufundishwa wala kuundwa kwa ajili ya kazi hizo.

Kielelezo cha akili bandia ya jumla

Mifumo ya sasa ya akili bandia hufanya kazi chini ya mipaka iliyowekwa na waundaji wake, mfano, mfumo wa akili bandia wa kutambua au kuunda picha hauwezi kutengeneza wavuti. Akili bandia ya jumla ni harakati ya kuunda mfumo wa akili bandia unaoweza kujiongoza, unaojitambua na wenye uwezo wa kujifunza ujuzi mpya. Wenye uwezo wa kutatua matatizo magumu katika mazingira na muktadha ambao haikufundishwa wakati wa uumbaji wake. [1]

Marejeo hariri

  1. "What is AGI? - Artificial General Intelligence Explained - AWS". Amazon Web Services, Inc. (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2024-01-10. 
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akili bandia ya jumla kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.