Al-Shymaa Kway-Geer
Al-Shymaa Kway-Geer (alizaliwa mwaka 1960) ni mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni mmoja kati ya wabunge wanawake 48 walioteuliwa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
Kway-Geer ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga nchini Tanzania na aliteuliwa kuwa mbunge mnamo mwaka 2008. Hapo awali Kway-Geer alikuwa mhudumu wa ndege[1]. Akiwa mlemavu wa ngozi (Albino), Kway-Geer ameonesha matumaini kwa watu wenye ulemavu kama yeye na kubadilisha mtazamo wa watu wengi nchini Tanzania wenye imani kuwa mtu mwenye ulemavu wa ngozi ni laana au chanzo cha kujipatia nguvu za giza. Manyanyaso kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yameshamiri sana nchini Tanzania yakiwemo mauaji ya maalbino, kuwavamia na kukata baadhi ya viungo vyao.
Angalia pia
hariri- Salum Khalfani Bar'wani (mtu wa kwanza mwenye ulemavu wa ngozi kuchaguliwa kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Tovuti ya Bunge la Tanzania
- Jeffrey Gettelman. "Albinos in Tanzania face deadly threat" in New York Times, June 8, 2008</ref>
- article on Kwegyir
- Washington Times article on Kwegyir
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |