Jakaya Kikwete
Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015.
Jakaya Mrisho Kikwete | |
Muda wa Utawala 21 Disemba 2005 – 5 Novemba 2015 | |
Makamu wa Rais | Ali M. Shein (2005–2010) Mohamed Bilal (2010–2015) |
---|---|
Waziri Mkuu | Edward Lowassa (2005–08) Mizengo Pinda (2008–2015) |
mtangulizi | Benjamin Mkapa |
aliyemfuata | John Magufuli |
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
| |
Muda wa Utawala 31 Januari 2008 – 2 Februari 2009 | |
mtangulizi | John Kufuor |
aliyemfuata | Muammar al-Gaddafi |
Muda wa Utawala Novemba 1995 – 21 Disemba 2005 | |
Rais | Benjamin Mkapa |
aliyemfuata | Asha-Rose Migiro |
Muda wa Utawala 1994 – 1995 | |
mtangulizi | Steven Kibona |
aliyemfuata | Simon Mbilinyi |
Mbunge wa Tanzania
wa jimbo la Chalinze | |
Muda wa Utawala Novemba 1995 – 2005 | |
aliyemfuata | Ramadhani Maneno |
tarehe ya kuzaliwa | 7 Oktoba 1950 Msoga, Tanganyika |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
chamakingine | TANU |
ndoa | Salma Kikwete |
watoto | 8 |
makazi | Ikulu, Dar es Salaam |
mhitimu wa | Chuo Kikuu cha Dar es Salaam |
Fani yake | Mchumi |
dini | Uislamu |
Military service | |
Allegiance | Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Service/branch | Jeshi la Tanzania |
Rank | Major |
Asili
Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.
Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.
Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.
Masomo
Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.
Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.
Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.
Kupanda ngazi katika siasa
1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.
Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.
Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.
Miaka kumi ya urais
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.
Kuapishwa kwa mara ya kwanza kwa Jakaya Kikwete kama Rais wa 4 wa Tanzania kulifanyika Jumatano, tarehe 21 Desemba 2005. Ilikuwa ni mwanzo wa muhula wa kwanza wa miaka mitano wa Jakaya Kikwete kama Rais na Ali Mohamed Shein kama Makamu wa Rais.
Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.
Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.
Heshima na Tuzo
Nishani
Nishani | Nchi | Tarehe | Ref | |
---|---|---|---|---|
Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu) | Uganda | Julai 2007 | [1] | |
Nishani ya Hilali Kijani ya Komori | Komori | Machi 2009 | [2] | |
Nishani ya Abdulaziz Al Saud | Saudi Arabia | Aprili 2009 | [3] | |
Nishani ya Ubora | Jamaika | Novemba 2009 | [4] | |
Nishani ya Oman (Daraja la Kwanza) | Omani | Oktoba 2012 | [5] |
Shahada za Heshima
Chuo Kikuu | Nchi | Shahada ya Uzamivu | Tarehe | Ref |
---|---|---|---|---|
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas (Minnesota) | Marekani | Daktari wa Sheria | 28 Septemba 2006 | [6][7] |
Chuo Kikuu cha Kenyatta | Kenya | Shahada ya Heshima | 19 Disemba 2008 | [8] |
Chuo Kikuu cha Fatih | Uturuki | Shahada ya Heshima katika Mahusiano wa Kimataifa | Februari 2010 | [9] |
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili | Tanzania | Daktari wa Afya ya Umma | Disemba 2010 | [10] |
Chuo Kikuu cha Dodoma | Tanzania | Shahada ya Heshima | 26 Novemba 2010 | [11] |
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam | Tanzania | Daktari wa Sheria | Oktoba 2011 | [12] |
Chuo Kikuu cha Guelph | Kanada | Daktari wa Sheria | 20 Septemba 2013 | [13][14] |
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania | Tanzania | Shahada ya Heshima | 21 Januari 2016 | [15] |
Marejeo
- Nyang'oro, Julius E. (2011). JK: A Political Biography of Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania. Trenton, NJ: Africa World Press, Inc. ISBN 1592217753.
Tanbihi
- ↑ "Museveni honours Nyerere", 10 July 2007. Retrieved on 26 Septemba 2013. (Kiingereza) Archived from the original on 2014-12-05.
- ↑ "Rais Kikwete, Jenerali Mwamunyange, Waziri Membe Watunukiwa Anjoun". Ikulu. 25 Machi 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-27. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "JK akiwa Saudia". Michuzi Blog. 16 Aprili 2009. Iliwekwa mnamo 26 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "President Kikwete Awarded Order of Excellence", 26 November 2009. Retrieved on 26 Septemba 2013. (Kiingereza) Archived from the original on 2013-09-27.
- ↑ "HM confers Oman Civil Order on Tanzania leader", October 2012. Retrieved on 26 Septemba 2013. (Kiingereza) Archived from the original on 2014-12-04.
- ↑ "President of Tanzania to speak here Sept. 28" (kwa Kiingereza). Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas (Minnesota). 25 Septemba 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Swallehe Msuya. "Tanzania's president touts country's progress at St. Thomas appearance", 30 September 2006. Retrieved on 25 Septemba 2013. (Kiingereza)
- ↑ "Kenyatta University Newsletter Vol. 4, Issue 15 (Special Graduation Edition)" (PDF) (kwa Kiingereza). Chuo Kikuu cha Kenyatta. 26 Januari 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-04-21. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ (in Kiingereza) Honorary Doctorate to the president of Tanzania from our university (Press release). Turkey: Chuo Kikuu cha Fatih. 19 February 2010. Archived from the original on 2012-12-24. https://web.archive.org/web/20121224011640/http://fatih.edu.tr/?basin_bultenleri%2C12&language=EN. Retrieved 25 Septemba 2013.
- ↑ "MUHAS Annual Report 2010-2011" (kwa Kiingereza). Chuo Kikuu cha Muhimbili. 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-09-30. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
- ↑ "JK, late Kawawa honoured at UDOM colourful, maiden graduation", 27 November 2010. Retrieved on 25 Septemba 2013. (Kiingereza)
- ↑ "JK atunukiwa udaktari wa sheria UDSM" (kwa Kiingereza). Michuzi Blog. 21 Ocotober 2011. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2013.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|trans_title=
ignored (|trans-title=
suggested) (help) - ↑ (in Kiingereza) U of G to Welcome Tanzanian President to Campus (Press release). Guelph, Canada: Chuo Kikuu cha Guelph. 18 September 2013. http://www.uoguelph.ca/news/2013/09/u_of_g_to_welcome_tanzanian_president.html. Retrieved 25 Septemba 2013.
- ↑ President of Tanzania at War Memorial Hall katika YouTube
- ↑ "Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atunukiwa shahada ya udaktari ya uhusiano wa kimataifa". 21 Januari 2016. Iliwekwa mnamo 1 Agosti 2020.
Viungo vya nje
- Jakaya Kikwete Fans Website Ilihifadhiwa 30 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.
- Government of Tanzania
- Ippmedia Interview with Col Kikwete Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- BBC Profile
- Jakaya Kikwete Swearing-In Ceremony
Alitanguliwa na Benjamin William Mkapa |
Rais wa Tanzania 2005-2015 |
Akafuatiwa na John Magufuli |