Allison Taylor
Allison Taylor ni jina la kuita uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika huu unachezwa na Cherry Jones, huyu ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Marekani, na amechukua nafasi kutoka kwa Bw. Noah Daniels katika siku ya ufunguzi wake, ambayo ilianza kuonekana katika sehemu ya 24: Redemption. Aliaza kuonekana rasmi akiwa kazini, ni baada ya kuanza kwa Msimu wa 7. Mume wake ni Henry Taylor, na mtoto wake wa kiume ni Roger Taylor (ambaye aliuawa kati ya sehemu za Redemption na Siku ya 7).
Allison Taylor | |
---|---|
muhusika wa 24 | |
Cherry Jones kama Allison Taylor | |
Imechezwa na | Cherry Jones |
Mionekano | Redemption, 7 |
Maelezo |
Katika uhusika
haririKabla ya kuchaguliwa kuwa kama Rais, Taylor alikuwa Seneta (kiti kilikuwa kikimilikiwa na baba yake). Amemshinda mgombea mwenzi Bw. Noah Daniels katika uchaguzi. Kwa mujibu wa maelezo ya Daniels, "kichwa cha maelezo" jilaumu kwa kushindwa na sio kupigania vilivyo ili ubaki kazini.