Ally Rehmtullah
Ally Rehmtullah (alizaliwa 18 Januari 1986) ni mbunifu wa mitindo wa Tanzania [1].
Maisha ya awali na kazi
haririNi Mtanzania wa kizazi cha nne mwenye asili ya Uhindi, ambaye alisoma katika shule ya Sanaa ya Baum na chuo cha Lehigh Valley, Marekani[2], kabla ya kurejea Tanzania kufanya kazi kama mwalimu wa sanaa ya picha mpaka alipobadili taaluma yake hadi kwenye ubunifu wa mitindo.
Mnamo Septemba 2008, alikuwa mbunifu wa kwanza wa Afrika Mashariki kufanya maonyesho ya mavazi katika London Fashion Week.