Sanaa
Sanaa (kutoka neno la Kiarabu) ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akili yake.
Vilevile sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa.
Kusanifu ni kuumba, kufanya jambo au kitu kwa kutumia ufundi/ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake. Mtu hueleza hisia zinazomgusa kwa kutumia umbo fulani ambalo limesanifiwa.
Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemewa ioneshe ufundi wa hali ya juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake.
Tunaweza kuona kazi ya sanaa kupitia tanzu za fasihi, uchoraji, ususi, ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi na kadhalika.
Kila umbo huwa na nyenzo zinazotumika katika kuliumba umbo hilo. Kwa mfano katika uchongaji kuna mti (gogo), panga, tezo, msasa, rangi na kadhalika.
Aina za sanaa
haririSanaa za maonyesho
haririHizi ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa, hivi kwamba uzuri wake ukaendelea kuonekana wakati wowote ule.
Hizi ni baadhi tu ya aina za sanaa ambazo hutoa umbo la kudumu:
Sanaa za vitendo
haririUzuri wa sanaa hizi umo katika umbo la vitendo, hivyo ilimradi kuupata uzuri huo ni lazima kutazama vitendo vinavyofanyika. Katika sanaa hizi lazima kuwe na chenye sifa kuu nne, ambazo ni:
- Dhana ya kutendeka (tendo)
- Mtendaji (fanani)
- Uwanja wa kutendea
- Watazamaji (hadhira)
Upekee wa fasihi
haririKati ya hizo, fasihi ni tanzu ya pekee kwa sababu zifuatazo:
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Cowan, Tyler (2008). "Arts". In David R. Henderson (ed.). Concise Encyclopedia of Economics (2nd ed.). Indianapolis: Library of Economics and Liberty.
. . http://www.econlib.org/library/Enc/Arts.html. – A look at how general economic principles govern the arts.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sanaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
,