Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel

Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel ni filamu ya mwaka wa 2009 kutoka nchini Marekani. Filamu inachanganya wahusika (live-action, yaani, wahusika binadamu na CGI wahusika vikatuni. Filamu ina mandhari ya ucheshi na ni mfululizo wa pili baada ya Alvin and the Chipmunks. Ndani yake anakuja Jason Lee, Zachary Levi, Anjelah Johnson, Wendie Malick, na David Cross. Filamu hii pia imeshirikisha sauti za nyota maarufu kama vile Justin Long, Matthew Gray Gubler, Jesse McCartney, Christina Applegate, Anna Faris, na Amy Poehler.

Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel
Imeongozwa na Betty Thomas
Imetayarishwa na Janice Karman
Ross Bagdasarian, Jr.
Imetungwa na Jon Vitti
Jonathan Aibel
Glenn Berger
Nyota Zachary Levi
David Cross
Jason Lee
Justin Long
Matthew Gray Gubler
Jesse McCartney
Christina Applegate
Anna Faris
Amy Poehler
Muziki na David Newman
Imehaririwa na Matt Friedman
Imesambazwa na 20th Century Fox
Imetolewa tar. 23 Desemba 2009
Ina muda wa dk. Dakika 89
Nchi Marekani
Lugha English
Bajeti ya filamu $75,000,000[1]
Mapato yote ya filamu $443,180,168[2]
Ilitanguliwa na Alvin and the Chipmunks (2007)

Filamu inashirikisha Alvin and the Chipmunks na wenzi wao wa kike waitwao The Chipettes. Filamu iliongozwa Betty Thomas, imetungwa na Jon Vitti, Jonathan Aibel, na Glenn Berger, imesambazwa na 20th Century Fox, na kutayarishwa na Regency Enterprises kwa ushirikiano wa Bagdasarian Productions. Awali ilipangwa itolewa mnamo tar. 19 Machi 2010, lakini badala yake ikahamishwa hadi tar. 23 Desemba 2009.

Hadithi

Wakati wa tamasha la kihisani la Chipmunks huko mjini Paris, Ufaransa, David Seville (Jason Lee) anajeruhiwa. Dave hana budi kujiuguza na analizimika kuwaacha Chipmunks chini ya uangalizi wa shanganzi yake. Mipango pia imefanywa ya wao kwenda shule. Baada ya ajali nyingine, wakina Chipmunks wameachwa chini ya uangalizi wa Toby (Zachary Levi), mjukuu wa shangazi yake Dave.

Muda huohuo, Ian Hawke (David Cross) anaishi chini ya kitako cha nyumba ya JETT Records. Machipmunks wa kike watatu, Brittany, Jeanette, na Eleanor, pia wanajulikana kama Chipettes, wanaungana na Ian anawakodi ikiwa kama mtego wa kurudi kwa Chipmunks na kufufua kazi yake.

Wakiwa shule, wakina Chipmunks wanazinguliwa na mizaha ya hapa na pale na baadaye kwenda ofisini kwa mkuu shule. Wanagundua kwamba mkuu wa shule ni mpenzi mkubwa wa Chipmunks na anawataka wasaidie msaada wa kifedha kwa ajili kusaidia kipindi cha muziki ambacho kipo hatarini kufa kwa kukosa fedha - hivyo waende kwenye shindano la muziki na wakishinda wataweza kusaidia kipindi hicho cha shule. Muda huohuo, wakati Ian anapokea gazeti lake la kila siku, anashtushwa kwa kukuta kina Chipmunks wapo katika ukurasa wa mbele. Baada ya kusoma habari zao, haraka akapeleka kina Chipettes shule.

Pale kina Chipmunks wanakutana na kina Chipettes, wameshangazwa kwa ufanano wao, lakini baada ya muda mfupi wakaanza uhasimu baada ya kugundua ya kwamba wapo na Ian. Wakina Chipmunks na Chipettes wanashindana kwa vita ya mabendi ili apatikane mshindi wa kwenye shindano, wakina Chipettes wameimba na Alvin ameshindwa kutokea kwenye onyesho kwa ajili ya Chipmunks - ambao baadaye wameadhibiwa. Pindipo Alvin anatokea, amekuta ukumbi mtupu na amepuuzwa na ndugu zake nyumbani.

Punde, wakina Chipettes wanakodiwa. Kwa bahati mbaya, tamasha hilo lipo usiku mmoja na lile la shule, hivyo Ian akaamua kubutulia mbali shindano la shule na kuwafanya kina Chipettes waimbe kwenye tamasha jipya. Wakati kina Chipettes wanakataa, anawatishia kuwapeleka kwenye mgahawa wa wauza mishikaki.

Huko shule, Alvin anapokea simu kutoka kwa Brittany na anaharakia kwenda kuwaokoa. Wakina Chipettes wanafanikiwa kutoroka na Alvin. Alvin na Chipettes wanawasili shindanoni na kuanza kuimba na hatimaye kushinda. Muda huohuo, Ian anaingia matatani zaidi pindi alipojaribu kujiigiza kama Chipettes kwenye tamasha lililoandaliwa kwa ajili ya wasichana. Dave anarudi wakati wa shindano na kuridhia kina Chipettes waishi pamoja.

Washirki

Kina Chipmunks

Kina Chipettes

Walionekaa

Marejeo

  1. Fritz, Ben (2009-12-28). "Holiday box-office take is highest in recent history". Los Angeles Times. Iliwekwa mnamo 2010-01-03.
  2. "Alvin and the Chipmunks: The Squeakquel Box Office". Box Office Mojo. Iliwekwa mnamo 2010-06-01.

Viungo vya Nje