Amani ni hali ya raha na salama bila ugomvi; ni kinyume cha fujo au vita.

Mara nyingi hali za amani ya nje na amani ya ndani hutofautishwa.

Amani ya nje au amani ya kisiasa na kijamii

hariri

Amani ya kisiasa ni hasa kutokuwa na vita na mapigano kati ya nchi mbalimbali au kati ya vikundi ndani ya jamii. Kama kuna mgongano kutokana na tofauti ya upendeleo juu ya jambo fulani amani inatunzwa kama pande zote zinafuata sheria au kanuni za jamii bila kutumia mabavu.

Mara nyingi maana kuu ya "amani" ni hali ya kutokuwa vita kati ya nchi kwa sababu vita huleta uharibifu mkubwa kushinda aina nyingine za ugomvi.

Amani inaweza kutaja pia tendo la kumaliza vita kwa njia ya mapatano kati ya washiriki wa vita au pia kati ya washindi na washindwa wakikubali kumaliza uadui. (linganisha Amani ya Westfalia).

Tangu vita kuu za dunia kulikuwa na majaribio mengi kuhakikisha amani kwa njia ya mapatano kati ya nchi zote za dunia. Shirikisho la Mataifa lilianzishwa mwaka 1919 likashindwa kuzuia vita kuu ya pili ya dunia ikafuatwa na Umoja wa Mataifa ulio na shabaha ya kupunguza na kuzuia vita kwa njia ya ushirikiano.

Tunatakiwa kulinda amani ili kusonga mbele hata kiuchumi.

Amani ya ndani au amani ya kiroho

hariri

Tangu kale watu waliona ya kwamba amani ya nje inaenda sambamba na amani ndani ya kila mtu. Penye hasira nyingi moyoni mwa watu ni vigumu kutunza amani ya nje.

Kwa sababu hiyo amani imekuwa jambo muhimu katika dini na falsafa.

Dini mbalimbali zina ujumbe kuhusu amani: