Amaury Nolasco
Amaury Nolasco (Amaury Nolasco Garrido amezaliwa tar. 24 Desemba 1970) ni mwigizaji anayejulikana sana kwa kuigiza kama Fernando Sucre kwenye tamthiliya Prison Break.
Amaury Nolasco | |
---|---|
Amezaliwa | Amaury Nolasco Garrido 24 Desemba 1970 |
Kazi yake | Mwigizaji |
Maisha ya awali
haririNolasco alizaliwa Puerto Rico, aliposoma baiolojia muda wote katika chuo cha Puerto Rico ili aje kuwa daktari. Kwa ufupi hakuwa na mpango wa kuja kuwa muigizaji. Baada ya kufanya shughuli ndogondogo za uigizaji, Nolasco alihamia New York, ambapo alipata mafunzo katika American British Dramatic Arts.
Rafiki wa utotoni wa Nolasco ni Jorge Posada, walikutana darasa la kwanza. Alifanya kazi kama kwenye klabu moja Los Angeles kama mhudumu.
Wasifu
haririPunde tu, Nolasco alishiriki katika tamthiliya kadhaa kama vile Arli$$, Crime Scene Investigation na ER. Alishiriki kwa mara ya kwanza kwenye filamu kama Orange Julius kwenye 2 Fast 2 Furious ya Universal. Baadae akashirikia kama Bernie Mac kwenye Mr. 3000.
Pia amecheza kwenye baadhi ya tamthilya na filamu kama George Lopez, CSI: NY na Benchwarmers. Ameuza sura kwenye Mind of Mencia, Aprili 29, 2007. Nolasco ameigiza kwenye filamu Transformers iliyoachiwa kwenye majira ya joto 2007. Lakini amefanya vizauri zaidi na kujitambulisha zaidi baada ya akuigiza kwenye tamthilia Prison Break ya FOX Network.
Nolasco ameuza sura kwenye video ya muziki Yes We Can ya Will.I.Am,[1] ambayo inaonesha kumuunga mkono mgombea urais wa marekani 2008, Barack Obama.
Magizo
haririFilamu
haririMwaka | Jina | Kama |
---|---|---|
2000 | Brother | Victor |
2002 | Final Breakdown | Hector Arturo |
2003 | The Librarians | G-Man |
2 Fast 2 Furious | Orange Julius | |
2004 | Mr. 3000 | Minadeo |
2006 | The Benchwarmers | Carlos |
2007 | Transformers | Figueroa |
2008 | Street Kings | Santos |
Max Payne | Jack Lupino | |
2009 | Armored | Palmer |
2011 | The Rum Diary | Segurra |
2013 | A Good Day to Die Hard | Murphy |
El Teniente Amado | Amado García Guerrero | |
2014 | In the Blood | Silvio Lugo |
2014 | Animal | Douglas |
2015 | Criminal |
Tamthiliya
haririMwaka | Jina | Kama |
---|---|---|
1999 | Arli$$ | Ivory Ortega |
Early Edition | Pedro Mendoza | |
2000 | The Dukes of Hazzard: Hazzard in Hollywood | Cypriano |
The Huntress | Flaco Rosario | |
2001 | CSI: Crime Scene Investigation | Hector Delgado |
2002 | ER | Ricky |
2003 | George Lopez | Young Manny |
2004 | Eve | Adrian |
2005 | CSI: NY | Ruben DeRosa |
2005 - present | Prison Break | Fernando Sucre |
2007 | Mind of Mencia | Amaury Nolasco |
2009 | CSI: Miami | Nathan Cole |
2010 | Southland | Detective Rene Cordero |
2010 | Chase | Marco Martinez |
2012 | Work It | Angel Ortiz |
2013 | Rizzoli & Isles | Rafael Martinez |
2013 | Burn Notice | Mateo |
2014 | Justified | Elvis Manuel Machado |
2014 | Gang Related | Matias |
TBA | Hot & Bothered | Rodrigo |
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Amaury Nolasco at the Internet Movie Database
- Amaury Nolasco katika Movies.com
- Wiki Page Ilihifadhiwa 7 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine.
- Amaury Nolasco's biography Ilihifadhiwa 5 Mei 2009 kwenye Wayback Machine. at Prison Break's official site