Amun alikuwa mmoja wa miungu wakuu katika dini ya Misri ya Kale. Aliabudiwa pamoja na mke wake Ament ( Amaunet ).

Amun

Ushuhuda wake Amun unapatikana tangu Himaya ya Kale ya Misri. Wakati wa nasaba ya 11 (karne ya 21 KK) Amun alikuwa mungu mkuu wa mji mkuu wa Thebi.

Kuunganishwa na miungu mingine hariri

Katika utawala wa Farao Ahmose (karne ya 16 KK) Amun alikuwa mungu wa kitaifa ilhali ibada yake iliunganishwa na ibada ya Ra akaabudiwa kwa jina la Amun-Ra.

Mwazoni aliabudiwa pale Thebi kama mungu wa upepo na mungu wa kuzaa akaendelea kutazamiwa kama mkuu wa miungu yote. na kumalizia mungu mkuu, na utajiri mwingi wa Misri uliowekwa wakfu kwa hekalu lake. Karibu na milenia ya pili KK, Thebi na ibada ya Amun ilikuwa na nguvu sana. Kadri utawala wa mafarao wa Thebi uliimarika pia katika maeneo mengine ya Misri, ibada za miungu iliyoabudiwa pale kuwa miungi mikuu iliunganishwa na ibada ya Amun. KWa njia Amun aliunganishwa mara nyingi na mungu wa Jua Ra na kuitwa Amun-Ra. Amun-Ra alisifiwa kama mungu wa kitaifa, muumbaji wa ulimwengu, mlinzi wa kibinafsi wa farao, na mungu wa vita.

Muumbaji hariri

Ilifikiriwa kuwa amejiumba mwenyewe na kisha akaumba kila kitu kingine akibaki mbali na ulimwengu wote. Kwa maana hiyo, alikuwa muumba asilia asiyeweza asiyegawanyika .

Amun alionyeshwa kwa umbo la kibinadamu, mara nyingi akiketi juu ya kiti cha enzi, na kuvaa kichwani taji nzito ambako linatoka manyoya mawili yaliyonyooka.

Marejeo hariri