Miungu (wingi wa mungu) ni jina linalojumlisha watu wanaoabudiwa na kuogopwa kama Mungu au vitu vyovyote visivyoweza kusikika wala kuonekana vinavyoabudiwa kama Mungu.

Katika utamaduni wa Kibantu hakuna wazo la miungu mingi. Katika mapokeo hayo Mungu ni mmoja tu, lakini kuwasiliana naye kulifanyika kwa njia ya mizimu hasa, si moja kwa moja.

Kumbe katika sehemu nyingi za dunia utamaduni wa asili ulikuwa na imani ya miungu mingi. Imani hizo zilipatikana hata katika mazingira ya taifa la Israeli, na pia wakati alipoishi Yesu, ingawa Wayahudi walishika imani yao ya pekee.

Dini za miungu mingi ("politeisimo") zilikuwa kawaida katika Afrika Kaskazini, Ulaya na sehemu nyingi za Asia kabla ya uenezaji wa Ukristo na Uislamu.

Kati ya miungu mingi iliyoabudiwa kila mmoja aliaminika kuwa na idara yake alipotawala hasa, kama vile hali ya hewa, vita, kifo, uponyaji, mavuno, mifugo, biashara, uzazi n.k.

Lugha ya Kiingereza inatunza mpaka leo kumbukumbu ya miungu mingi iliyoabudiwa katika utamaduni wa Ulaya wa Kale kabla ya kuingia kwa Ukristo. Majina ya siku za juma ni majina ya miungu ambayo siku ziliaminiwa kuwa chini ya ulinzi wao hasa.

Kumbe miungu iliyomaanisha nyota au sayari, kama vile Jua, Mwezi na Saturn ilikuwa mapokeo ya Roma, si asili ya Uingereza.

Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Miungu kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.