Misri ya Kale

Misri ya Kale ni ustaarabu uliokuwepo Afrika kaskazini, sambamba na mto Naili, kuanzia kwenye delta au mdomo wa Naili, toka kaskazini mwa Misri kwenda kusini hadi Jebel Barkal, kwenye maporomoko ya nne, wakati wa kupanuka kwake (Karne ya 15 KK).

Piramidi ya Giza pamoja na Sphinx.
Ufalme wa Misri ya Kale mnamo 1500 KK pamoja na maeneo iliyotawala.

Ustaarabu huo ulidumu kwa karibu milenia tatu, toka takribani mwaka 3000 KK hadi mwaka 30 KK nchi ilipovamiwa na Waroma na kuwa sehemu ya Dola la Roma.

Uti wa mgongo wa Misri ya Kale ulikuwa mto Naili. Sehemu kubwa ya nchi hiyo ni jangwa lakini umwagiliaji wa mashamba kwa njia ya maji ya mto ulileta mazao mazuri yaliyolisha watu wengi.

Mahitaji ya kupanga na kutunza mifereji pamoja na mitambo ya umwagiliaji na kusimamia ugawaji wa maji yalisaidia kutokea kwa vyanzo vya hisabati na mwandiko. Mwandiko wa Misri ulikuwa hiroglifi zilizokuwa aina ya mwandishi wa picha.

Dini ya Misri ilitarajia maisha baada ya kifo ambayo yanapaswa kuandaliwa na watu wakati wa maisha haya.

Wafalme, walioitwa Mafarao, walijengewa makaburi makubwa sana na piramidi ni kati ya makaburi makubwa kabisa duniani.

Duniania ya Kale ya Misri;

 • Nubia
 • Kush
 • Napata
 • Thebes
 • Memphis
 • Giza
 • Gezira
 • Saqara
 • Luxor
 • Aswan
 • Kom Ombo
 • Sinai
 • Mt. Katarina
 • Abu Simbel
Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Misri ya Kale kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.