Andrew Mwenda (alizaliwa Fort Portal, 1972) ni mwandishi wa habari wa Uganda.

Andrew Mwenda, 2008

Yeye alihudhuria Chuo cha Busoga Mwiri mashariki mwa Uganda kabla ya kuhudhuria Chuo Kikuu cha Makerere. Alikamatwa na kutolewa na dhamana na serikali ya Uganda kwa ajili ya "kumiliki vifaa na kuchapisha makala ya uchochezi ".[1] Alipata shahada ya bwana ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha London nchini Uingereza. Awali alikuwa mhariri wa siasa wa gazeti la Monitor na mwenyeji wa kipindi cha Andrew Mwenda Live katika redio ya KFM . Mwaka wa 2005, alikuwa miongoni mwa waandishi wa habari kumi na sita walioalikwa na serikali ya Uingereza kukutana na waziri mkuu Tony Blair kommande kujadili ripoti ya Tume ya Afrika.

Agosti mwaka wa 2005 alishatakiwa kwa fitna kwa utangazaji mjadala wa sababu ya kifo cha makamu wa rais wa Sudan John Garang. Garang aliuawa wakati helikopta ya rais wa Uganda ilianguka katika eneo nyuma kutoka nchini Uganda. Katika kipindi chake cha redio, mwandishi aliishutumu serikali ya Uganda "ktokuwa makini" na alisema kuwa walikuwa walimweka Garang helikopta isiyokuwa taratibu ... usiku ... katika hali ya hewa isiyokuwa nzuri ... juu ya eneo hatari".[2] Alimshutumu pia Rais Yoweri Museveni, na kumwita mshindwa, anayeogopa na "mtu aliyetoka kijijini", na kusema siku za rais zimehesabiwa ikiwa yeye "akiendeleza mgongano nami".[3]

Mnamo Julai mwaka wa 2006, Mwenda alionekana mbele ya kamati ya British House of Commons katika umasikini wa dunia ili kushuhudia dhidi ya misaada Afrika. Ameandika sana juu ya madhara ya misaada katika mchakato wa maendeleo katika Afrika na kuchapishwa katika magazeti ya kifahari kama International Herald Tribune na Der Spiegel na kufanyika redio na televisheni ya BBC katka somo hili. Bwana Mwenda pia ametajwa katika vyombo vya habari vya kimataifa - BBC, CNN, New York Times, Washington Post, The Times, The Economist, na magazeti mengine mengi,mitandao ya redio na televisheni, katika Ulaya na Amerika Kaskazini.

Pia amekosoa mashirika ya misaada kwa kusema nikutowajibika na kuchangia katika ufisadi. Yeye anaamini kuwa misaada ya magharibi haijasaidia kwa maendeleo ya Afrika, kwani huendeleza ufisaadi na vita. Anasema kuwa misaada inakwenda katika nchi zisizohitaji misaada, nchi ambazo zina watu walioaguka, kuliko zile ambazo zimejirekebisha. Mwezi Juni wa 2007, yeye alitoa hotuba kuhusu masuala haya katika mkutano TED Arusha, Tanzania.

Bwana Mwenda alikuwakatika ushirika wa John S. Knight katika chuo kikuu cha Stanford nchini Marekani. Mnamo Desemba mwaka wa 2007, alizinduwa gazeti lake la The Independenet mjini Kampala.

Makala

hariri

Andrew Mwenda: Hebu tuchukue mwamko mpya wa misaada ya Afrika

Makala ya Karibuni

hariri
  • 2007: Investieren Geht über Schmieren, Entwicklungspolitik, Desemba 2007, Nr. 12 62 Jahr.
  • 2007: nguvu binafsi nchini Uganda, Makala ya Demokrasia, Julai 2007, Volume 18, Number 3
  • 2006: "Kuendeleza Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini: Jinsi Uganda iliepuka k zogo"; katika ushambulzi wa Umasikini Afrika : Uzoefu kutoka mashinani,kuhaririwa na Louise Fox na Bob Liebenthal, Benki ya Dunia, Washington DC.
  • 2006: Misaada kutika nje inamaliza Uwajibikaji wa Kidemokrasia Uganda (jarida la Taasisi ya Cato, katika mkutano wa think tank Washington DC.
  • 2006: Akiwa na Roger Tangri: 'Siasa, Wafadhili, na kutowajibika kwa Taasisi za Kupambana na Ufisadi nchini Uganda', Jrida la Modern African Studies, 44, 1 (2006)
  • 2005: Akiwa na Roger Tangri: ' Siasa, Marekebisho ya Wafadhili , na ushirikiano nchini Uganda', African Affairs, 104, 416 (2005), 449-67.
  • 2003: Akiwa na Roger Tangri: "Ufisadi katika jeshi na Siasa Rush Uganda tangu mwishoni mwa miaka ya 1990." Katika Review of African Political Economy No 98, 2003.
  • 2001: Akiwa na Prof Roger Tangri, Ufisadi nchini Uganda katika Ubinafsishaji katika miaka ya 1990, Afrika Affairs 100-398 (2001) 87-103

Marejeo

hariri
  1. AllAfrica.com, retrieved 2008/5/1
  2. AlertNet.Org, retrieved 2008/5/1
  3. Reuters, Ilihifadhiwa 18 Januari 2006 kwenye Wayback Machine. retrieved 2008/5/1