Dkt John Garang de Mabior (23 Juni 1945 - 30 Julai 2005) alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan na kiongozi wa zamani wa waasi wa Sudan People's Liberation Army.

John Garang de Mabior


Muda wa Utawala
9 Januari 2005 – 30 Julai 2005
Makamu wa Rais Salva Kiir
aliyemfuata Salva Kiir

Muda wa Utawala
9 Januari 2005 – 30 Julai 2005
Rais Omar al-Bashir
mtangulizi Ali Osman Taha
aliyemfuata Salva Kiir
Vacant until 11 Agosti 2005

tarehe ya kuzaliwa 23 Juni 1945
Bor (Jonglei, Sudan)
tarehe ya kufa 30 Julai 2005 (umri 60)
New Site (Southern Sudan, Sudan)
chama SPLM
ndoa Rebecca Nyandeng De Mabior

Miaka ya Awali

hariri

Kutoka kabila la Wadinka Garang alizaliwa katika familia maskini katika kijiji cha Wanglei huko Bor, Sudan, katika ukanda wa upper Nile ya Sudan (kwa sasa Jonglei State). Kwa kuachwa yatima akiwa na umri wa miaka kumi, alilipiwa karo ya shule na mmoja wa jamaa zake, na kwenda shule Wau na kisha Rumbek. Mwaka wa 1962 alijiunga na vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe Sudan lakini kwa sababu alikuwa mchanga sana, viongozi walimshauri yeye na wenzake kutafutilia elimu. Kwa sababu ya mapigano yaliyokuwa yakiendelea, Garang alilazimishwa kuhudhuria elimu yake ya Sekondari nchini Tanzania. Baada ya kushinda udhamini, aliendelea na kuweza kupata shahada ya BA katika uchumi mwaka wa 1969 kutoka Grinnell College, Iowa, USA. Huko alijulikana sana kwa kupenda vitabu kwake. Alipewa udhamini mwingine kufanyaa masomo hitimu katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, lakini akachagua kurudi Tanzania na kusomea Uchumi wa kilimo katika Afrika Mashariki kama Thomas J. Watson Fellow katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Akiwa UDSM, alikuwa mwanachama wa University Students' African Revolutionary Front. Hata hivyo, punde Garang aliamua kurejea Sudan na kujiunga na waasi[onesha uthibitisho]. Kuna ripoti nyingi za makosa zinazodai kwamba Garang alikutana na kufanya urafiki na Yoweri Museveni, rais wa baadaye wa Uganda, wakati huu; ingawaje Garang na Museveni walikuwa wanafunzi wa UDSM katika miaka ya 1960, hawakuhudhuria wakati mmoja[1].

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilimalizika baada ya Mkataba wa Addis Ababa wa 1972 na Garang, kama waasi wengine, aliwekwa katika jeshi la Sudan. Kwa miaka kumi na moja, alifanya kazi kama askari na kupanda kutoka safu ya Kapteni hadi Kanali baada ya kufanya Infantry Officers Advanced Course katika Fort Benning, Georgia. Katika kipindi hiki alichukua ruhusa ya kimasomo ya miaka minne na akapata Shahada ya Masters katika Uchumi wa Kilimo na Ph.D. katika uchumi kutoka Iowa State University, baada ya kuandika Thesis juu ya maendeleo ya kilimo ya Sudan Kusini. Kufikia 1983, Knl Garang alikuwa akitumika kama mwalimu mwandamizi katika Shule ya jeshi iliyokuwa Wadi Sayedna kilomita 21 kutoka kitovu cha (Omdurman) ambapo aliwaelekeza makadeti kwa zaidi ya miaka 4 na baadaye yeye akateuliwa kutumika katika idara ya kijeshi katika idara ya utafiti wa kijeshi katika Makao Makuu ya Jeshi mjini Khartoum.

Kiongozi wa waasi

hariri

Mwaka wa 1983, Garang alikwenda Bor, kwa minajili ya kupatanisha askari wa serikali ya kusini wapatao 500 katika Battalion 105 ambao walikuwa wakipinga kuwekwa doria katika vituo vya kaskazini. Hata hivyo, Garang tayari alikuwa mmoja wa baadhi ya maafisa waliokuwa na njama katika amri ya Kusini kwa ajili ya kupanga kuhama Battalion 105 na kuunga mkono waasi waliopinga serikali. Wakati serikali iliposhambulia Bor mwezi wa Mei, Battalion ilijitoa nje, Garang akaenda kwa njia nyingine na kujiunga nao katika ngome ya waasi nchini Ethiopia. Kufikia mwisho wa Julai, Garang alileta askari waasi zaidi ya 3000 chini ya utawala wake kupitia vuguvugu mpya la Sudan People's Liberation Army / Movement (SPLA / M), ambalo lilikuwa linapinga utawala wa kijeshi na kutwaliwa kwa sehemu kubwa ya nchi na Uislamu, na kuzihimiza ngome nyingine za jeshi kuasi dhidi ya sheria ya Kiislamu juu ya nchi na serikali[2]. Hatua hii ilikuwa ndio mwanzo unaokubaliana wa Vita Kuu vya Pili vya weneyewe kwa wenyewe vya Sudan, ambavyo vilisababisha vifo milioni mmoja na nusu katika kipindi cha miaka ishirini ya migogoro. Ingawa Garang alikuwa Mkristo na eneo kubwa la kusini mwa Sudan sio la Waislamu (wengii ni animist), mwanzoni hakuzingatia masuala ya kidini ya vita.

SPLA ilipata msaada wa Libya, Uganda na Ethiopia. Garang na jeshi lake walidhibiti sehemu kubwa ya mikoa ya kusini mwa nchi, iliyoitwa Sudan Mpya . Yeye alidai kuwa 'ujasiri wa askari wake kutoka kwa "uthibitisho kwamba sisi tunapambana vita vya haki. Hilo ni jambo ambalo Sudan Kaskazini na watu wake hawana. " Wakosoaji walipendekeza motisha za fedha kwa uasi wake, wakibainisha kuwa kiasi kikubwa cha mafuta ya Sudan kiko katika kusini mwa nchi.

 
Garang katika umati wa wafuasi

Garang alikataa kushiriki katika serikali ya mpito mwaka wa 1985 au uchaguzi wa 1986, na kubaki akiwa kiongozi wa waasi. Hata hivyo, SPLA na serikali zilitia saini mkataba wa amani tarehe 9 Januari 2005 mjini Nairobi, Kenya. Tarehe 9 Julai 2005, aliapishwa kama makamu wa rais, cheo cha pili kwa ukuu katika nchi, kufuatia sherehe ambapo yeye na Rais Omar al-Bashir walitia saini katiba ya kugawana madaraka. Yeye pia alikuwa kiongozi wa utawala wa kusini mwa Sudan yenye uhuru mdogo kwa miaka sita kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya uwezekano wa Kuganywa. Hakuna Mkristo au mtu kutoka kusini aliwahi kushikilia cheo cha juu kama hicho serikalini. Akizungumza baada ya sherehe, Garang alisema, "Mimi nawapongeza watu wa Sudan, hii si amani yangu au amani ya al-Bashir, ni amani ya watu wa Sudan."

Kama kiongozi, sifa za kidemokrasia za John Garang zilitiliwa mashaka mara nyingi. Kwa mfano, kulingana na Gill Lusk "John Garang hakuvumilia upinzani na mtu yeyote aliyehitilafiana naye aidha alifungwa jela au kuuawa"[3].. Chini ya uongozi wake, SPLA ilishutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu[3].

Itikadi za SPLA zilikuwa za uvuli kama Bw Garang mwenyewe. Aligeuka kutoka kwa mrengo wa Marxism hadi kupata msaada kutoka kwa Wakristo wenye siasa kali kutoka Marekani[3].

Idara ya Taifa ya Marekani ilisema kuwa kuwepo kwa Garang katika serikali kungesaidia kutatua Mgogoro wa Darfur magharibi mwa Sudan, lakini wengine waliona madai haya kuwa "matumaini kupita kiasi". [4]

Mwishoni mwa Julai 2005, Garang alikufa baada ya ndege ya rais wa Uganda aina ya helikopta Mi-172 aliyokuwa akisafiria kuanguka. Alikuwa anarudi kutoka mkutano wa Rwakitura na mshirika wake wa muda mrefu Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Hakuiambia serikali ya Sudan kwamba alikuwa anaenda mkutano huu na hivyo basi hakuchukua ndege ya rais. Shirika la televisheni la kitaifa kwanza lilisema kuwa ndege iliyombeba Garang ilikuwa imetua salama, lakini Abdel Basset Sabdarat, Waziri wa Habari wa nchi, alikwenda kwenye televisheni masaa kadhaa baadaye kukataa ripoti hiyo. Kwa kweli, ilikuwa ni Yasir Arman, msemaji wa SPLA / M ndiye aliiambia serikali kuwa ndege iliyombeba Garang iliwasili salama ili kuokoa muda kwa ajili ya mipangilio ya ndani katika SPLA kabla ya kifo chake kujulikana.Ndege ya Garang ilianguka siku ya Ijumaa na hivyo ilibakia kuwa iliyotoweka hadi Jumamosi iliyofuata na wakati huu wote serikali ilidhani bado alikuwa Sudan Kusini. Mapema baadaye, taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Sudan Omar el-Bashir alithibitisha kuwa helikopta ya rais wa Uganda ilianguka katika "mojawapo ya mlima iliyoko kusini mwa Sudan kwa sababu ya kutoona vizuri na kusababisha kifo cha Dkt John Garang De Mabior, wenzake sita na wafanyikazi saba wa ndege hiyo ya Uganda." [1]Mwili wake ulibebwa kwa ndege hadi New Site, makazi yaliyoko kusini mwa Sudan karibu na eneo la ajali, ambamo wapiganaji waasi wa zamani na wafuasi raia walikusanyika kutoa heshima zao kwa Garang. Mazishi ya Garang yalifanyika tarehe 3 Agosti mjini Juba.[5] Mjane wake, Nyandeng Rebecca De Mabior, aliahidi kuendelea na kazi yake akisema "Katika utamaduni wetu sisi husema, ukimuua simba dume, utaona atakachofanya simba wa kike." [6]

Maswali kuhusu kifo

hariri
 
Garang akipunga mkono muda mfupi kabla ya kifo chake.

Serikali ya Sudan na kiongozi wa SPLA walilaumu hali ya hewa kwa ajali hiyo. Hata hivyo, kuna tashwishi katika ukweli wa jambo hili, hasa miongoni mwa safu-na-faili za SPLA. Yoweri Museveni, rais wa Uganda, anadai kwamba uwezekano wa "sababu za nje" kuhusika usingeweza kuondolewa[onesha uthibitisho].

Athari kwa amani

hariri

Akionekana kuchangia pakubwa katika kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, madhara ya kifo cha Garang kwa mpango wa amani yalikuwa wazi. Serikali ilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, ambayo hayakuzuia vurugu kubwa mjini Khartoum na vifo vya angalau vijana 24 hivi kutoka Sudan Kusini waliowashambuliwa watu kutoka Sudan kaskazini na kupigana na vikosi vya usalama. Baada ya siku tatu za ghasia, vifo viliongezeka hadi kufikia 84 [2] Migogoro pia iliripotiwa katika maeneo mengine ya nchi. Viongozi wakuu wa SPLM, pamoja na Halifa wa Garang Salva Kiir Mayardit, walisema kwamba mchakato wa kutafuta amani ungeendelea. Wachambuzi walipendekeza kwamba kifo kingeleta aidha demokrasia mpya ya uwazi katika SPLA, ambayo baadhi ya watu walikosoa kwa kuongozwa sana na Garang, au kuzuka kwa vita vya wazi kati ya makundi mbalimbali ya kusini yaliyokuwa yameletwa pamoja na Garang.

Maandishi yake

hariri
  • Garang, John, 1987 John Speaks . M. Khalid, ed. London: Kegan Paul International.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Prunier, Gérard (2009). Africa's World War: Congo, the Rwandan Genocide, and the Making of a Continental Catastrophe. Oxford: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-537420-9. s. 80
  2. [4] ^ Johnson, D. The Root of Sudan's Civil Wars , Indiana University Press, 2003, uk. 61-2.
  3. 3.0 3.1 3.2 BBC: obituary: John Garang
  4. Reeves, Eric (2005-08-02). "Untimely Death". The New Republic.
  5. "Sudan bids rebel leader farewell". BBC News. 2005-08-06.
  6. Wax, Emily (2005-08-30). "Widow of Sudan's Garang Steps In to Continue His Mission". The Washington Post. Iliwekwa mnamo 2007-04-25.

Marejeo

hariri
  • Aufstand in der Dreistadt na Thomas Schimidinger katika Jungle World Nr.32: 10 Agosti 2005; ISSN 1613-0766

Viungo vya nje

hariri