Angel Nyigu

Mcheza densi na mwandishi wa chore wa Tanzania

Angel Bathlomeo Nyigu (maarufu kama "Angel Nyigu"; amezaliwa 10 Disemba 1999) ni Mchezaji wa densi na mkufunzi wa densi kutoka Tanzania. Yupo chini ya kampuni ya Wasafi Classic Baby(WCB).[1]

Angel Nyigu akiwa katika ukumbi wa mazoezi wa Tanzania Dance na wanafunzi wake.

Mbali na kuwa Wasafi, wakati mwingine hufanya minenguo huru na wasanii wengine. Amewahi kuonekana katika video ya Polepole ya Makihiyo.[2]

Angel ni mnenguaji wa kwanza kijana kuifanya kazi hiyo kama sehemu ya ajira rasmi nchini Tanzania.[3]

Marejeo

  1. "Dansa wa WCB Angel Nyigu afunguka: Kufanya kazi na Diamond ni ngumu sana (Video)". Bongo5.com (kwa American English). 2020-10-28. Iliwekwa mnamo 2021-06-08.
  2. Makihiyo - Pole Pole (Official Dance Video), iliwekwa mnamo 2021-06-08
  3. Welle (www.dw.com), Deutsche, Angel Nyigu msichana aliyepata mafanikio kwenye Dansi | DW | 22.01.2021, iliwekwa mnamo 2021-06-08