Antonov An-225
An-225 Mriya ni ndege ya Ukraine iliyokuwa kubwa kuliko zote duniani miaka ya 1988 hadi 2019. Ina injini sita. Ilitengenezwa na kampuni ya Antonov. Ilipangwa kwa shughuli za mradi wa usafiri wa anga-nje wa Umoja wa Kisovyeti.
Ndege ya kwanza ilikamilishwa mwaka 1988, nakala ya pili ilianzishwa bila kumaliza kutokana na kuporomoka kwa Umoa wa Kisovyeti mwaka 1989 [1].
Ndege ya pekee iliyokwisha iliwahi kupimzishwa kwa miaka kadhaa[2] lakini ilirudishwa kuanzia 2001[3].
Matumizi yake ni ghali kwa hiyo haina ratiba ya kawaida inakodiwa pekee kama kuna haja kubeba mizigo mikubwa sana. Uwezo wake ni kubeba tani zaidi ya 253[4].
Mwaka 2019 taji la ndege kubwa zaidi limechukuliwa na Stratolaunch Roc.
Marejeo
hariri- ↑ The worlds biggest plane may have a new mission, tovuti ya BBC 5 Mai 2017
- ↑ An-225 (An-225-100) ""Мрiя"", Antonov OKB (NATO Cossack) Archived 31 Oktoba 2015 at the Wayback Machine., taarifa kwenye tovuti ya ram-home.com
- ↑ Laster der Lüfte, taarifa kwa Süddeutsche Zeitung (Kijerumani) "Lori la hewani", tar.22 Oktoba 2012, [www.aspapress.com/downloads/SZ_Spaeth_Antonow.pdf online hapa]
- ↑ An-225 (An-225-100) ""Мрiя"", Antonov OKB (NATO Cossack), tazama chanzo juu
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |