Areopago(kutoka Kigiriki Ἄρειος Πάγος) ni mwamba uliotokeza juu ya Akropoli ya Athens, mji mkuu wa Ugiriki.

Areopago inavyoonekana kutoka Akropoli.
Upande wa kulia unaonekana ubao ulioandikwa hotuba ya Mtume Paulo katika Areopago (Mdo 17).

Ilitumika kama mahakama[1] na kama mahali pa midahalo ya kifalsafa.

Kwa sababu hiyo Mtume Paulo alipotaka kuhubiri Ukristo alialikwa kwenye Areopago. Hotuba hiyo maarufu inapatikana katika Mdo 17.

"Areopago mamboleo" inamaanisha mitandao na vyombo vya habari ambavyo ni uwanja mpya wa kuwasiliana na kueneza mawazo kati ya watu wa nyakati hizi.

Tanbihi hariri

  1. Atheneion Politeia. Perseus Tufts. Iliwekwa mnamo 8 February 2016.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Areopago kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.