Athini (pia: Athene kwa Kigiriki Αθήνα "Athina") ni mji mkuu wa Ugiriki (Uyunani), mji mkubwa wa nchi hiyo, na mojawapo kati ya miji mashuhuri ya dunia yenye historia ndefu ya miaka elfu kadhaa.

Majengo ya Akropoli juu ya kilima iliyokuwa boma na mtaa wa mahekalu ya Athens ya Kale. Huko Mtume Paulo alitoa hotuba maarufu (Mdo 17).

Siku hizi mji una wakazi milioni 3.

Jina limetokana na mungu wa kike "Athena" aliyeabudiwa kama mungu wa elimu na wa vita zamani za Ugiriki wa Kale.

Historia

hariri

Katika karne kabla ya Kristo Athens ulikuwa mji muhimu uliotawala sehemu kubwa ya Ugiriki pamoja na miji mingi hadi Italia na Uturuki ya leo.

Athens ilikuwa maarufu kwa wataalamu wake, hasa wanafalsafa kama Sokrates, Plato na Aristoteles.

Kisiasa inaitwa asili ya demokrasia.

Baadaye ilikuwa chini ya utawala wa Dola la Roma na tangu mwaka 1453 chini ya Dola la Uturuki. Hapo mji ukawa hauna umuhimu wowote, hivi kwamba wakati wa uhuru wa Ugiriki mwaka 1834 ulikuwa na wakazi wapatao 1000 tu.

Tangu hapo umekuwa mji mkuu wa Ugiriki ukakua tena.

Michezo ya kwanza ya Olimpiki ya kisasa ilifanyika Athens mwaka 1896. Michezo ilirudi tena kufanyika huko mwaka 2004.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Athens kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.