Aslay Isihaka Nassoro

mwanamuziki wa Tanzania
(Elekezwa kutoka Aslay)

Aslay Isihaka Nassoro (maarufu kama Dogo Aslay; alizaliwa 6 Mei, 1995) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania.

Aslay
Jina la kuzaliwaAslay Isihaka Nassoro
Amezaliwa6 Mei 1995 (1995-05-06) (umri 28)
Kazi yakeMwimbaji
AlaSauti

Maisha hariri

Alianza kufahamika kuanzia mwaka 2011 baada ya kutoa kibao chake cha Nakusemea alichokitoa akiwa chini ya Mkubwa Fella. Kabla ya hapo, alitoa wimbo mwingine uitwao Niwe Nawe akiwa amemshirikisha Temba. Baadaye akatoa nyimbo nyingine kadhaa kabla ya kujiunga na bendi ya vijana ya Yamoto Band.

Akiwa ndani ya bendi hiyo, alionesha uwezo mkubwa wa kuimba, akiwa na wenzake, Beka Flavour, Maromboso na Enock Bella. Nyimbo alizoshiriki kutunga na kuimba akiwa Yamoto Band ni pamoja na Yamoto (Nitajuta), Cheza Kwa Madoido, Mama, Nisambazie Raha na nyingine nyingi.

Yamoto Band haikudumu sana ambapo ilianza 2013/2014 hadi 2017 ilipovunjika kwa sababu mbalimbali na wasanii waliokuwa kwenye kundi hilo kuanza kufanya kazi zao kwa kujitegemea. Kuanzia 2017, Aslay akiwa msanii wa kujitegemea chini ya meneja wake wa zamani, Chambuso, alianza upya kung'ara.[1]

Akiwa msanii wa kujitegemea, ametoa nyimbo nyingi mfululizo hali ambayo imechanganya wengi, lakini mwenye alielezea kwanini amefanya ni kwa sababu hana nyimbo nyingi alizofanya akiwa msanii wa kujitegemea zaidi ya zile alizokuwa na Yamoto Band[2]

Ili asiimbe za Yamoto akiwa kwenye matamasha, kaamua kutoa nyimbo nyingi. Nyimbo hizo ni pamoja na Angekuona, Usiitie Doa akiwa na Khadija Kopa, Muhudumu, Baby, Likizo, Pusha Natamba na Huna. Awali ilitazamika kama Mkubwa Fella ndiye hasa mmiliki wa muziki wa kizazi kipya, lakini kupitia Aslay, Chambuso anasema si lazima yeye ndiye awe meneja bora wa muziki huu.[3]

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aslay Isihaka Nassoro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.