Audrey Blignault

Mwandishi wa Afrika Kusini

Audrey Bettie Blignault (6 Julai, 19161 Oktoba, 2008) alikuwa mwandishi kutokea nchini Afrika Kusini.

Audrey Blignault
Faili:Audrey Blignault.jpg
Nchi Africa kusini
Kazi yake Mwandishi

Maisha yake

hariri

Binti wa mama kutokea Ireland na baba Mwafrikana ambaye alikuwa meya wa jiji, Audrey Bettie Swart alizaliwa huko Bredasdorp. Alisomea fasihi ya Kiafrikana katika chuo cha Stellenbosch na kupata shahada ya uzamili katika sanaa ya lugha za Afrikana na Kiholanzi.

Mwaka 1940, alianza kufundisha huko Wellington, baadaye Stellenbosch. Mwaka 1945, akawa mhariri wa Die Huisvrou, jarida la masuala ya wanawake. Mwaka huohuo, alianza programu katika redio mahususi kwa ajili ya kitabu chake cha kwanza kwa lugha ya Afrikaana. Kwa kipindi cha miaka 25, ameandika Makala nyingi katika jarida ya wanawake wa Afrikana kwa jina la Sarie. Insha kutoka katika Makala hizo zilikusanywa na kuchapishwa katika vitabu 17. Mkusanyo wa barua zake kama Audrey Blignault: ’n Blywende vreugde ulichapishwa mnamo Mei 2008.[1] Blignault alikua pia ni mhariri wa Naweekpos na alikuwa mkurugenzi wa kipindi cha wanawake na utamaduni katika kituo cha redio cha Afrika Kusini.[2]

Blignault alifariki katika zahanati ya Cape Town akiwa na umri wa miaka 92.[3]

Familia

hariri

Aliolewa mara mbili: Mara ya kwanza na Andries Blignault; ambaye alifariki katika ajali ya gari mwaka 1967. Yeye mwenyewe alipata majeraha makubwa katika ajali hiyo, na ndiye pekee aliyenusurika kufa. Aliolewa na bwana Attie de Villiers mnamo mwaka 1970.[1]

Tuzo na Heshima

hariri

Alipokea tuzo za ‘’Eugène Marais’’ mnamo mwaka 1961, ‘’W.A. Hofmeyr’’ mwaka 1965 na ‘’Adelaide Ristori’’. Mwaka 1982, alipata tuzo ya heshima ya raisi wa nchi kwa huduma ya hali ya juu. Alikua mwanamke wa kwanza kutajwa katika bodi ya shule ya sayansi na utamaduni wa Afrika kusini.[3][2]

Kazi zilizoteuliwa

hariri
  • In klein maat Kaapstad, 1955.
  • Die vrolike lied (1957)
  • Met ligter tred (1962)

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Audrey Blignault:Prolific essayist", October 5, 2008. 
  2. 2.0 2.1 "Audrey Blignault". Skrywers in Afrikaans (kwa Kiafrikana). Mieliestronk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-09. Iliwekwa mnamo 2021-04-17.
  3. 3.0 3.1 "Writer Audrey Blignault dies aged 92", October 1, 2008.