A.Y. (mwanamuziki)

Mwanamuziki na mfanyabiashara wa Tanzania
(Elekezwa kutoka Ay)

Ambwene Alen Yesaya (anajulikana zaidi kama AY; alizaliwa Mtwara, tarehe 5 Julai 1982) ni msanii mashuhuri wa muziki wa Komesho, Rap, na Hip Hop, mwigizaji, na mwanamitindo kutoka Tanzania.

Ambwene Yesaya

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Ambwene Alen Yesaya
Amezaliwa 5 Julai 1982 (1982-07-05) (umri 42)
Asili yake Mtwara, Tanzania
Aina ya muziki Bongo Flava, hip-hop
Kazi yake

AY ameacha alama kubwa katika tasnia ya muziki nchini kwa nyimbo zake maarufu kama Raha tu 1-2, Raha Kamili, Machoni kama Watu, na Binadamu, miongoni mwa nyingine nyingi.

Umaarufu wake haukuishia Tanzania pekee; AY anafahamika pia katika nchi za jirani kama Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na hata Kusini mwa Afrika. Hapo awali, alikuwa mwanachama wa kundi maarufu la East Coast Team, ambalo liliongozwa na Gwamaka Kaihula (King Crazy GK) pamoja na Khamis Mwinjuma (Mwana FA au Mwana Falsafa). Kundi hili lilikuwa na makao yake eneo la Upanga, jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa, AY anaishi nchini Marekani, ambako anaendelea na shughuli zake za muziki na mitindo. Katika safari yake ya muziki, AY pia aliwahi kushirikiana na ndugu wawili kutoka Nigeria wanaounda kundi la P-Square, hatua ambayo iliongeza upekee na hadhi ya kazi zake kimataifa.

Albamu Alizotoa

hariri
  1. Raha Kamili (2003)
  2. Hisia Zangu (2005)
  3. Habari ndiyo hiyo (2008)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu A.Y. (mwanamuziki) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.