Ayaan Hirsi Ali
Ayaan Hirsi Ali (kwa Kisomali: Ayaan Xirsi Cali: Ayān Ḥirsī 'Alī; alizaliwa: Ayaan Hirsi Magan, huko Somalia, 13 Novemba 1969)[1] ni mwanaharakati wa haki za wanawake, mwandishi, msomi na mwanasiasa wa zamani raia wa Uholanzi na Marekani.[2][3]
Alipata usikivu wa kimataifa kwa kuwa mkosoaji wa Uislamu na mtetezi wa haki za wanawake wa Kiislamu, akipinga kwa nguvu ndoa za kulazimishwa, mauaji ya heshima, ndoa za utotoni na ukeketaji wa wanawake.[4][5]Alianzisha shirika la kulinda haki za wanawake liitwalo AHA Foundation. Ayaan Hirsi Ali hufanya kazi kwa ajili ya Hoover Institution na American Enterprise Institute.[6][7]
Mnamo mwaka 2003, Hirsi Ali alichaguliwa kuwa mwanachama wa baraza la wawakilishi la Uholanzi.
Baba yake Ayaan Hirsi Ali, Hirsi Magan Isse, alikuwa mwanachama muhimu wa Somali Salvation Democratic Front na kiongozi katika mapinduzi ya Somalia. Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake, baba yake alifungwa gerezani kwa sababu ya kupinga serikali ya Kijamaa ya Siad Barre.
Baba yake Hirsi Ali alikuwa msomi na mpinzani wa serikali, pamoja na kuwa Muislamu mcha Mungu. Aliwahi kusoma nje ya nchi na alipinga vikali ukeketaji wa wanawake. Lakini wakati baba yake akiwa gerezani, bibi yake Hirsi Ali alimleta mwanaume kufanya ukeketaji huo akiwa na umri wa miaka mitano. Kwa bahati nzuri, bibi yake hakumpata mwanamke wa kufanya ukeketaji, kwani inasemekana kwamba unakuwa "mpole zaidi" ukifanywa na wanaume.
Marejeo
hariri- ↑ "Ayaan Hirsi Ali". Britannica. https://www.britannica.com/biography/Ayaan-Hirsi-Ali.
- ↑ "Ayaan Hirsi Ali on Q&A: the west must stop seeing Muslims only as victims", The Guardian, 16 May 2016.
- ↑ "Ayaan Hirsi Ali's 'Heretic'", The New York Times, 1 April 2015.
- ↑ "Ayaan Hirsi Ali: "You can't change these practices if you don't talk about them"", The New York Times, 24 February 2017.
- ↑ "Ayaan Hirsi Ali on Conversations with Bill Kristol".
- ↑ "Ayaan Hirsi Ali".
- ↑ "Ayaan Hirsi Ali". American Enterprise Institute - AEI (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2020-08-
13.
{{cite web}}
: Check date values in:|access-date=
(help); line feed character in|access-date=
at position 9 (help)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ayaan Hirsi Ali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |