Kisomali ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Somalia, Ethiopia, Kenya na Jibuti inayozungumzwa na Wasomali.

Kupitia kwa Wasomali wahamiaji, Kisomali huzungumzwa katika nchi nyingine nyingi kama vile Kanada, nchi mbalimbali za Ulaya na za Uarabuni.

Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisomali nchini Somalia ilihesabiwa kuwa watu 8,340,000. Pia kuna wasemaji 4,610,000 nchini Ethiopia (2007), 2,386,222 nchini Kenya (2009), na 297,200 nchini Jibuti (2006).

Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisomali kiko katika kundi la lugha za Kikushi.

Viungo vya nje Edit

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisomali kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.