Bab el Mandeb (kiarabu: باب المندب "Mlango wa machozi") ni mlango wa bahari uliopo kati ya nchi ya Jibuti upande wa Afrika na Yemeni upande wa Asia.

Picha ya Bab el Mandeb kutola Angani kati ya Jibuti na Yemen
Bab el Mandeb

Mlango wa bahari una upana wa 27 km ukiunganisha Bahari ya Shamu na Bahari Arabu kupitia Ghuba ya Aden. Bab el Mandeb iko kati ya njia za bahari duniani zinazotumiwa sana na meli kwa sababu usafiri wote kati ya Ulaya na Asia kwa njia ya Mfereji wa Suez hupita humo.

Ndani ya mlango upande wa Yemen kipo kisiwa cha Perim penye mnara wa taa. Ni sehemu ya Yemen. Upande wa pwani la Kiafrika kuna funguvisiwa ndogo ya "Kaka Saba" au Visiwa vya Sawabi ambavyo ni sehemu ya Jibuti.