Guba ya Aden ni mkono pana wa Bahari Hindi kati ya Somalia upande wa kusini na Rasi ya Uarabuni upande wa kaskazini. Inaanza kwenye sehemu ya Bahari Hindi iitwayo pia Bahari Arabu na kuelekea kwa mlango wa bahari wa Bab el Mandeb unaoiunganisha na Bahari ya Shamu.

Mahali pa Ghuba ya Aden


Eneo, visiwa, nchi na miji ya pwani

hariri

Ghuba hii ina urefu wa kilomita 1,000 na upana wake ni kati ya 150 km hadi 440 km. Kimo cha maji hufikia urefu wa mita 3,748. Imepakana na nchi za Yemen, Somalia (au Somaliland) na Jibuti.

Mabandari muhimu zaidi ni Aden nchini Yemen, Berbera nchini Somalia na mji wa Jibuti nchini Jibuti.

Kuna funguvisiwa viwili:

Jiolojia

hariri

Kijiolojia ghuba ya Aden ni sehemu ya kaskazini ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki linaloendelea hapa chini ya uso wa bahari.

Bahari ya maharamia

hariri

Siku hizi ghuba hii ni kati ya njia za bahari hatari kwa usafiri kwa meli kwa sababu ya maharamia wenye vituo vya hasa Somalia lakini pia Yemen. Manowari za kimataifa zinajaribu kulinda eneo hili.