Bahari ya Siberia Mashariki

Bahari ya Mashariki ya Siberia (rus. Восто́чно-Сиби́рское мо́ре vostochno-sibirskoye more) ni bahari ya pembeni ya Bahari ya Aktiki, kaskazini kwa Urusi. Eneo lake ni 944.600 km².

Bahari ya Mashariki ya Siberia
Pevek ni bandari kuu kwenye bahari ya Mashariki ya Siberia, picha ilipigwa wakati wa mwezi wa Januari 2008

Iko kati ya visiwa vya Siberia Mpya upande wa magharibi na Kisiwa cha Wrangel kwa mashariki upande wa kaskazini ya pwani la Siberia, kati ya Bahari ya Laptev na Bahari ya Chukchi.

Kati ya tabia zake ni tabianchi baridi sana, maji yenye chumvi kidogo, uhaba wa uoto, wanyama na wakazi wa kibinadamu, uwingi wa barafu inayoyeyuka kwenye miezi ya Agosti – Septemba pekee.

Wakazi asilia walikuwa makabila ya kienyeji wawindaji, wavuvi na wafugaji wa reindeer. Leo hii walio wengi ni Warusi. Kazi yao inapatikana hasa katika migodi na kama mabaharia. Mji mkubwa ni bandari la Pevek ambayo ni mji kaskazini zaidi ya Urusi bara mwenye wakazi 4,721.[1][2][3][4][5].

Tanbihi

hariri
  1. William Elliott Butler Northeast arctic passage (1978) ISBN 90-286-0498-7, p. 60
  2. Forsaken in Russia's Arctic: 9 Million Stranded Workers, NYTimes, January 6, 1999
  3. From Vancouver to Moscow Expedition Ilihifadhiwa 18 Julai 2011 kwenye Wayback Machine., Yakutia Today
  4. History of Pevek Ilihifadhiwa 6 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine., Pevek web portal (in Russian)
  5. Polar bear strays onto Chukotka runway Ilihifadhiwa 4 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine., Vladivostok News, Issue 338 November 22, 2002.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Siberia Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.