Bamba la Ufilipino

Bamba la Ufilipino (ing. Philippine Plate) ni bamba la gandunia mojawapo lililopo chini ya bahari ya Pasifiki. Liko chini ya sehemu ya bahari iliyopo upande wa kaskazini-mashariki ya visiwa vya Ufilipino.

Ramani ya bamba la Ufilipino

Upande wa mashariki wake Bamba la Pasifiki linasukumwa chini ya Bamba la Ufilipino. Mwendo huu umesababisha kutokea kwa mifereji ya bahari kama vile ya Bonin, Mariana, Yap na Palau. Mpaka na Mfereji wa Mariana kipande kimeanza kuvunjika na wakati mwingine hutajwa kama bamba la pekee kwa jina la Bamba la Mariana[1].

Upande wa kaskazini bamba hili linazamishwa chini ya visiwa vya Japani na hapa kugongana na Bamba la Ulaya-Asia. Hali hii ni sababu ya kutokea kwa mitetemeko ya ardhi mikali nchini Japani.


Tanbihi

hariri
  1. Bird, P. (2003). "An updated digital model of plate boundaries". Geochemistry, Geophysics, Geosystems. 4 (3): 1027. doi:10.1029/2001GC000252.

Marejeo

hariri
  • Robert Hall, Jason R. Ali, Charles D. Anderson, Simon J. Baker: Origin and motion history of the Philippine Sea Plate. Tectonophysics, vol. 251, no 1–4, 1995, pp. 229–250, ISSN 0040-1951 doi:10.1016/0040-1951(95)00038-0