Bamba la Pasifiki ni kati ya mabamba makubwa ya gandunia ya dunia yetu. Lipo chini ya bahari ya Pasifiki ikiwa ni bamba la gandunia kubwa kabisa. Maada yake ni miamba mizito ya gumawesi.

Bamba la Pasifiki kwa rangi ya kahawia nyeupe
Pete ya moto au mstari wa volkeno huzunguka mipaka ya Bamba la Pasifiki; mistari ya buluu ni sehemu penye volkeno nyingi.

Mipaka

hariri

Bamba la Pasifiki hupakana na mabamba ya Amerika ya Kaskazini, Juan Fuca, Cocos, Nazca, Antaktika, Australia na Ufilipino.

Mwendo na pete ya moto

hariri

Bamba lote lina mwendo wa kuelekea kaskazini-magharibi kwa kasi ya sentimita 10 kwa mwaka.

Mwendo huo unaacha nafasi upande wa mashariki inayoonekana kama bonde la ufa kwenye sakafu ya bahari. Upande wa magharibi bamba linajisukuma chini ya bamba la Ufilipino na tokeo lake ni mfereji wa Mariana.

Kando ya bamba kuna volkeno nyingi zinazoitwa "pete ya moto".