Barack Hussein Obama Sr. (18 Juni 1934 - 24 Novemba 1982) alikuwa mchumi mkuu wa serikali ya Kenya. Alikuwa baba wa Barack Obama, rais wa arobaini na nne wa Marekani.

Barack Obama Sr.
Amezaliwa Baraka Obama
18 Juni 1934
Wilaya ya Rachuonyo, Kenya
Amekufa 24 Novemba 1982
Nairobi, Kenya
Elimu Chuo Kikuu cha Hawaii

Chuo Kikuu cha Harvard

Maisha ya awali

hariri

Barack Obama Sr. alizaliwa mwaka 1934 katika Wilaya ya Rachuonyo, mwambao wa Ziwa Viktoria, nchini Kenya. Wakati wa utoto wake, aliishi katika kijiji cha Nyang'oma Kogelo, Wilaya ya Siaya, Mkoa wa Nyanza. Familia yake ni watu wa kabila la Wajaluo.

Baba yake aliitwa Onyango Obama na mama yake aliitwa Habiba Akumu Nyanjango. Baba yake na mama yake walikuwa na watato wawili wa kike na mtoto mmoja wa kiume, Barack Obama Sr. Akumu na Onyango walitengana na Akumu aliiacha familia mwaka 1945. Baada ya Akumu kuacha familia, mke wa tatu wa Onyango alimlea Barack Obama Sr. na dada zake.

Ndoa na familia

hariri

Obama alimuoa Kezia Aoko katika sherehe ya kikabila katika nchi ya Kenya mwaka 1954. Walipata watoto wawili, Malik na Auma. Baadaye, Obama alioa wanawake wengine wawili. Mmoja wa wanawake alikuwa Stanley Ann Dunham, mwanamke Mmarekani. Dunham alikuwa na mtoto, ambaye baadaye alikua rais wa Marekani, Barack Obama. Baadaye walitengana tarehe 20 Machi 1964.

Mwaka 1959, Obama alipata ufadhili wa masomo ya uchumi kutoka kwa Tom Mboya. Udhamini ulitoa elimu katika nchi za Magharibi kwa wanafunzi wa Kenya. Mwaka 1959, Obama alienda Chuo Kikuu cha Hawaii na kuwa mwanafunzi wa kwanza wa kigeni wa Afrika wa chuo kikuu hicho. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Hawaii baada ya miaka mitatu na digrii ya uchumi.

Mwezi wa tisa mwaka 1962, Obama alisafiri mpaka mji wa Cambridge, jimbo la Massachusetts, nchi ya Marekani na kuendelea kusoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Harvard. Alipata digrii nyingine ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Harvard mwaka 1965.

Miaka ya mwisho na mauti

hariri

Mzozo wa Obama na rais wa Kenya, Jomo Kenyatta, uliharibu kazi yake. Aliingia katika tuhuma baada ya Tom Mboya kuuawa mwaka 1969 kwa sababu Mboya alikuwa mshauri wake. Jomo Kenyatta alimfukuza kazi Obama, hivyo haikuwezekana kwa Obama kupata kazi. Barack Obama Sr. alipata ajali mbili za gari na kupoteza miguu yote miwili. Halafu, alianza kukabiliana na umaskini na unywaji pombe. Mwaka 1982, alipata mtoto mwingine. Lakini miezi sita baadaye, Barack Obama Sr. alikufa katika ajali ya gari huko Nairobi. Watu wengi mashuhuri wa kisiasa walienda kwenye mazishi yake.

Marejeo

hariri