BAKIZA
(Elekezwa kutoka Baraza la Kiswahili Zanzibar)
BAKIZA ni kifupi cha Baraza la Kiswahili la Zanzibar. Baraza hili liliundwa mnamo mwaka 1983.
Majukumu makuu ya BAKIZA ni pamoja na kukuza maendeleo ya Kiswahili katika funguvisiwa la Zanzibar, kusimamia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili katika Baraza la Wawakilishi na katika vyombo vya habari, kama vile magazeti, redio na televisheni, kutunga kamusi na majarida kwa Kiswahili sanifu na fasaha, kupitia na kusanifu maandishi ya Kiswahili kwa matumizi mbalimbali kama vile katika ofisi za serikali na watu binafsi. Kutafsiri kazi mbalimbali kutoka katika lugha nyingine kama vile Kiingereza na Kiarabu na kuziweka katika Kiswahili sanifu na fasaha.