Kamusi za Kiswahili
Kamusi ya Kiswahili-Kiswahili (kamusi wahidiya)
Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza (kamusi thania)

Kamusi (kutoka neno la Kiarabu قاموس qamus) ni kitabu ambacho kinaorodhesha maneno ya lugha yaliyokusanywa kutoka kwa watumiaji wa lugha fulani, kwa mfano lugha ya Kiswahili.

Maneno hupangwa kwa mtindo wa alfabeti, hutoa maana, asili na ufafanuzi wa utumizi wa maneno na jinsi yanavyotumika au yanavyotamkwa.[1]


Aina za kamusiEdit

Kuna aina mbalimbali za kamusi ambazo ni:

 1. Kamusi wahidiya yaani ya lugha moja ambako maneno yanapangwa na kuelezwa kwa lugha ileile (mfano: Kiswahili-Kiswahili)
 2. Kamusi thania yaani ya lugha mbili ambako maneno ya lugha moja yanaorodheshwa halafu maana huonyeshwa kwa lugha tofauti, mfani ni Kiswahili-Kiingereza, au Kiingereza-Kiswahili
 3. Kamusi elezo (ing. encyclopedia) inayolenga kukusanya maelezo ya mambo ambayo yanatajwa kwa maneno. Wikipedia ni kamusi elezo ya kwanza kwa Kiswahili.

Muundo wa kamusiEdit

Kimuundo kamusi imegawanyika katika sehemu kuu tatu:

 1. Utangulizi wa kamusi
 2. Matini ya kamusi
 3. Sherehe ya kamusi/hitimisho

1. Utangulizi wa kamusiEdit

Hii ni sehemu ya kwanza ya kamusi, sehemu hii hujumuisha muhtasari wa sarufi ya lugha yenyewe pamoja na maelezo ya namna ya kutumia kamusi.

2. Matini ya kamusiEdit

Hii ni sehemu yenye vidahizo vyote vya kamusi husika, kuanzia alfabeti a-z vidahizo vyote huorodheshwa hapa na kufafanuliwa.

3. Sherehe ya kamusiEdit

Ni taarifa zinazoingia mwishoni mwa kamusi.

Faida za kamusiEdit

 • Kamusi hutusaidia kujua misamiati mipya.
 • Kamusi hutusaidia kujua aina za maneno, kwa mfano kitenzi.
 • Kamusi hutusaidia hata kwa wale watu ambao hawajui lugha, k.mf. Kiswahili.
 • Kamusi huelezea zaidi kuhusu maneno. Kwa mfano: tembo - kisawe chake ni ndovu.
 • Kamusi hutusaidia kujua lugha ya kigeni, kwa mfano Kifaransa
 • Kamusi hutusaidia kusoma hata kwa wale wasiojua kusoma, kwa sababu kamusi huwa na michoro au picha.

Dhima ya picha katika kamusiEdit

Michoro (au picha) katika kamusi ina faida zifuatazo:

 • husaidia wale wasiojua kusoma;
 • husaidia kuelewa kwa undani zaidi maana ya neno.

MarejeoEdit

 1. * Masuko Christopher Saluhaya, 2013. ISBN 978 9987 9581 1 5.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit


  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamusi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.