Bartolomea Riccoboni
Bartolomea Riccoboni (takriban 1369 – 1440) alikuwa mtawa wa Kidominiko katika monasteri ya Corpus Domini huko Venezia, Italia.
Aliandika kumbukumbu ya kihistoria ya monasteri hiyo na orodha ya kumbukumbu za wafu (necrology). [1] Amechunguzwa kama mfano mzuri wa mwanzo wa maandishi ya wanawake katika mashirika ya ombaomba ya karne za kati za mwisho.[2]
Mbali na masuala yanayohusiana na monasteri yake, pia alirekodi matukio ya Farakano la Kanisa la Magharibi, ambapo alikuwa mfuasi wa Papa Gregori XII.
Marejeo
hariri- ↑ Daniel Bornstein, Life and Death in a Venetian convent, University of Chicago Press, 2000.
- ↑ Graeme Dunphy, "Perspicax ingenium mihi collatum est: Strategies of authority in chronicles written by women", in Juliana Dresvina, Authority and Gender in Medieval and Renaissance Chronicles, Cambridge Scholars Publishing: Cambridge, 2012 (online).
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |