Venezia (pia: Venisi kutokana na Kiingereza Venice) ni mji wa Italia na makao makuu ya mkoa wa Veneto, kaskazini-mashariki mwa nchi.

Venezia
Venezia is located in Italia
Venezia
Venezia

Mahali pa Venezia katika Italia

Majiranukta: 45°26′00″N 12°20′00″E / 45.43333°N 12.33333°E / 45.43333; 12.33333
Nchi Italia
Mkoa Veneto
Wilaya Venizia
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 270,660
Tovuti:  http://www.comune.venezia.it/
Maboti ya gondola mjini Venezia
Kitovu cha Venezia kwa jicho la ndege
Mfereji mkuu wa "Canale Grande"
Mifereji ni kama barabara

Venezia ni mji wa pwani uliojengwa kwenye visiwa vidogo 117 ndani wa wamba la Venezia. Visiwa hivi vinakaa karibu kiasi kwamba madaraja 400 yanaunganisha mifereji kati yake. Mifereji ndani ya mji ni kama barabara na sehemu kubwa ya usafiri ni kwa maboti madogo.

Mji umekua kupitia eneo la visiwa tu na mwaka 2006 wakazi 269,000 walihesabiwa; 92,000 waliishi visiwani na wengine barani.

Venezia ni mji wa kale wenye umri wa karibu miaka 1,500. Jamhuri ya Venezia ilikuwa dola lenye nguvu katika Mediteranea kwa sababu ilikuwa na manowari nyingi na vituo vya kijeshi kwenye visiwa vingi vya Mediteranea. Msingi wa nguvu yake ulikuwa biashara ya baharini na utajiri wake. Venezia ilikuwa kiungo cha kibiashara kati ya Ulaya ya Kikristo na dunia ya Kiislamu.

Ilikuwa jamhuri ya kujitawala kabisa kwa karne nyingi hadi mwaka 1797 ilipovamiwa na Napoleon na kuunganishwa kwanza na Italia na baadaye na Austria. Tangu 1866 imekuwa sehemu ya Italia.

Kutokana na historia hii ya utajiri mji umejaa majengo mazuri na kazi za sanaa zinazovuta watalii kwa mamilioni kila mwaka kutoka kila upande wa dunia. Venezia iko katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Venezia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.