Basseterre
Basseterre ni mji mkuu wa shirikisho la Saint Kitts na Nevis ambalo ni nchi ya visiwani ya Antili Ndogo kwenye Bahari Karibi. Idadi ya wakazi ni takriban 15,500 (2005).
Mji wa Basseterre (Saint Kitts na Nevis) | |
Utawala | Shirika raia za Saint George na Saint Peter |
Anwani ya kijiografia | Latitudo: 17°18′N Longitudo: 62°44′W |
Kimo | 15 m juu ya UB |
Eneo | 6.1 km² |
Wakazi | - mji: 15,500 (2005) |
Msongamano wa watu | watu 2,541 kwa km² |
Simu | +1869 (nchi yote) |
Mahali | |
Mjini kuna kitovu cha kiuchumu wa visiwa, uwanja wa ndege na viwanda vya sukari.
Mwimbaji Joan Armatrading alizaliwa Basseterre kabla ya kuhamia Uingereza na wazai wake akiwa mtoto.
Historia
haririBasseterre iliundwa na Wafaransa 1627 ikawa mji mkuu wa koloni ya Kifaransa ya St. Christophe. 1627 pamoja na kisiwa chote ilitwaliwa na Uingereza.
Basseterre iliharibiwa kabisa mara kadhaa kutokana na vita, matetemeko ya ardhi, tufani na moto.