Latitudo
Latitudo (kwa ing.: latitude) ni mahala pa mchoro wa dunia au ramani huonyesha kwa mistari iliolazwa ni njia ya kuonyesha mahali duniani kwa kutaja umbali wake kutoka ikweta kwa kipimo cha digrii (°).
Mahali penye ikweta kamili (kwa mfano Nanyuki katika Kenya) ina latitudo ya "0". Mahali pa mbali ni ncha ya kaskazini au ya kusini zinazotajwa kwa 90°. Pamoja na kipimo cha longitudo inataja mahali kamili duniani.
Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north) na "S" (south) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).
Digrii za latitudo hugawiwa katika umbali wa 60 dakika au minuti; dakika ya latitudo ni mita 1852 au maili moja ya kibahari. Dakika hugawiwa katika nukta au sekondi. Mfano: 13°19.717′ N.
Latitudo muhimu ni:
1. Ikweta (0°)
2. Tropiki ya kansa (23½°Kas)
3. Tropiki ya kaprikoni (23½°Kus)
4. Duara la aktiki (66½°Kas)
5. Duara la antaktika (66½°Kus)
Pamoja na namba ya longitudo inaonyesha mahali kamili kwenye uso wa dunia.