Saint Kitts na Nevis


Saint Kitts na Nevis ni nchi ya visiwani kwenye visiwa viwili vya Bahari ya Karibi na nchi ndogo kabisa ya Amerika yote.

Saint Kitts na Nevis


Ramani ya St. Kitts na Nevis

Mji mkuu wa Basseterre uko kwenye kisiwa cha Saint Kitts. Kisiwa kidogo cha Nevis (kutoka jina la zamani la Kihispania: Nuestra Señora de las Nieves) kipo km 3 kusini-mashariki kwa Saint Kitts.

Zamani pia kisiwa cha Anguilla kiliunganishwa na visiwa hivi kuwa koloni moja la Uingereza.

Watu hariri

Wakazi ni 54,961: wengi wana asili ya Afrika (75.1%) au ni machotara Wafrika-Wazungu (12.3%).

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini ile ya kawaida ni Krioli.

Upande wa dini, 82.4% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Waanglikana na Wamethodisti.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons


Serikali
Taarifa za jumla
Ramani
Utalii
Habari
  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Saint Kitts na Nevis kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.